April 20, 2013

MAFURIKO YALIYOTOKEA WILAYA YA NYASANa Hoops Kamanga, Mbamba Bay

Mnamo tarehe 14 mwezi huu, kulitokea maafa makubwa yaliyosababishwa na mvua iliyonyesha katika maeneo mbambali wilayani Nyasa katika mkoa wa Ruvuma. Kama tunavyojua kuwa wilaya hiyo inasehemu kubwa ya ukanda wa ziwa nyasa, hivyo wahanga wa mafuriko hayo ni wakazi wa ukanda wa nyasa. 

Kama tulivyosema mwanzoni kwamba haya ni maafa makubwa na ahaykuwahi kutokea katika kipindi chochote kwani yameacha hasara kubwa kwa jamii za wanyasa. Kwa kipindi cha miaka ya nyuma kuliwahi kutokea maafa hayo yaliyosababishwa na kimbunga lakini hakukuwa na hasara kubwa kama hii. 

Kulingana na rekodi ambazo zinapatikana wilayani hapa, mpaka sasa maafa hayo ya mafuriko usiku wa kuamkia tarehe 14/04/2013, kuna hasara mbalimbali kama ifuavyo;
1. Mtu mmoja  amefariki dunia katika kijiji cha Ndengere, nje kidogo ya mji Mbamba Bay
2. Ng’ombe 7 wamesombwa na maji huku ikipatikana zaidi ya mizoga 6.
3. Mamba wamesombwa watatu wamesombwa kutoka mtoni kwenye mashamba ya mpunga karibu na makazi ya watu. 
4. Jumla ya hekari 87 za mpunga zimeharibika kabisa na mafuriko hayo katika vijiji vya Mbamba bay, Kilosa na Ndesule. 


 

No comments:

Post a Comment

Maoni yako