December 22, 2008

Nimerudi, Nimepona jamani


Ni saa 1 na dakika 10, naadika haya haraka haraka {angalia picha kutoka ugonjwani hiyo}. Nimepiga maana kaka Fadhy Mtanga anasema wanyasa hatujui kupiga picha ha ha ha ha ha. Nimerejea jamani baada ya kuwa kando kwa siku kadhaa maana apangalo maulana hakuna wa kulizuia, malaria yanibana sana nikashindwa hata kufanya mazoezi ya kukimbia kama dada Yasinta {much respect sister. Malaria yalinifanya niwe kama mwehu muda wote nachukia. Nawashukuru walionipa faraja na kunijulia hali yangu, msijali sana PAMODA DAIMA, dada Yasinta asante na wengine, kama jina lako halipo hapa naweka ....................... ili ujaze jina lako. Watu wangu wa nyasa maanake naona walidhani jamaa kaacha blogu. Sivyo waungwana siwezi nasema siwezi maana blogu kwangu ni TULIZO LA MOYO mmm najua mtakumbusha mashairi niliyokwisha kuyaimba hapa jinsi ninanyomzimia mtu fidodido ha ha ha ha ha. bila kumsahau rafiki yangu mkubwa Fita Lutonja, Redrose Janeth {we belong together} mola akulinde zaidi

5 comments:

 1. pole sana kwa homa, maana unaonekana umekwisha kweli. hilo ndio tatizo la kuishi nyasa samaki watamu lakini sasa malaria . ha ha haaaaa oh nina maana pole sana

  ReplyDelete
 2. Pole kwa kuugua. Mwenyezi Mungu akujalie afya njema na baraka tele.
  Karibu tena!

  ReplyDelete
 3. Pole sana mkuu kwa homa x-mas njema na mwaka mpya tuombe ufike salama uwe wa peace duniani kote amin.

  ReplyDelete
 4. asanteni nyoooooote, naamini tupo pamoja daima

  ReplyDelete

Maoni yako