December 17, 2008

naipenda sana picha hii

dada Mary Mbunda akiwa katika shughuli za nyumbani. Yuko pale Lituhi kwa rafiki yangu mkubwa RAYMOND NDOMBA {much Respect Brother} najua tupo pamojadaima kama samaki na maji au mizizi na ardhi Mkuu

7 comments:

 1. napenda sana maisha ya kiafrika naipenda sana afrika yangu. maisha mazuri na ya raha

  ReplyDelete
 2. Najua maisha ni mazuri,
  Lakini ninaitaka sababu,
  Kwanini picha hiyo ni nzuri,
  Waungwana nipeni majibu.

  ReplyDelete
 3. Picha imedaka vizuri shughuli za kina mama wengi Afrika katika kuhakikisha msosi unafika mkekani kwa walaji.

  Kuhusu maisha ya kiafrika ni mazuri na raha, siwezi kumshangaa Dada Mary Mbunda akikataa .

  Katika silika ya binadamu kuhangaikia kurahisisha shughuli. Dada Mbunga angeweza kufurahia mashine ya kisasa kuliko kinu na ungo.

  Swali:
  Hivi kama mMoroko na mKenya wote ni Waafrika, maisha ya kiafrika ni yapi?

  ReplyDelete
 4. Picha zako zinaelezea uhalisi wa maisha ya mwambao wa Ziwa Nyasa. Kwa vile nimetembelea baadhi ya sehemu hizo, kwa mfano Mbamba Bay, nazithamini sana na kuzifurahia picha hizi, kwani zinanikumbusha mengi. Nakutakia maendeleo mema katika shughuli hii muhimu.

  ReplyDelete
 5. Asante kaka Simon, lakini swali lako gumu kweli kweli labda nimwombe mzee wa changamoto atusaidie hilo na watu wangu wote nao wajibu Mmoroko na Mkenya maisha ya kiafrika ni yepi?

  Mzee wa Mbele, nashukuru sana kunitembelea mkuu, naamini yapo mambo ambayo yananipa simazni lakini inatakiwa kuyakabili haya na mengine. TUNAWEZA na hakika TUTAWEZA LEO. karibu tena

  ReplyDelete
 6. Jamani hivi huo sio unga wa mhogo? Unanikumbusha kwetu jamani.... nsima ya mayao na mbelele(somba).

  Zikomu!!!

  Mama Malaika
  UK

  ReplyDelete
 7. umeniumbusha Lundu jamani,nakumbuka tulitokea mbaha kwenda lundu kupanda meli ya Mv Songea ilikuwa mwaka 1991 da si mchezo nakupenda sana kunyumba.

  ReplyDelete

Maoni yako