NA
MWANDISHI WETU
KAMA
ulidhani ni binadamu pekee anajenga nyumba na kupangisha utakuwa unajidanganya
kwa kuwa mwambao mwa ziwa Nyasa katika Kijiji cha Mtupale kata ya Chiwanda,kuna
aina ya ndege anayeitwa Fundichuma (Hamerkop) ambaye anajenga nyumba na
kupangisha kwa ndege na viumbe wengine kama mijusi.
Afisa
Maliasili na Utalii wa Mkoa wa Ruvuma Afrikanus Challe ambaye pia ni mzaliwa wa
mwambao mwa ziwa Nyasa anasema ndege huyo anapenda kuishi jirani na ziwa au mto
kwa sababu chakula chake kikuu ni samaki.
Challe
anabainisha kuwa Fundi chuma ni ndege wenye uwezo wa kujenga nyumba kubwa yenye
vyumba vingi juu ya mti na kwamba ndege hao jike na dume wanapendana sana na
kwamba huwa hawaachani hadi mmoja anapokufa.
Kwa
mujibu wa Challe,ndege hao wanajenga nyumba kubwa na kukaribisha ndege wengine
na viumbe wengine ambao hupenda kuishi katika nyumba hizo kutokana na ulinzi wa
ndege hao.
Hata
hivyo Challe anasema kwa utamaduni wa makabila ya watu wa mwambao mwa ziwa
Nyasa ndege huyo wanamheshimu sana kutokana na ustarabu wake hivyo wanalinda
makazi yake ili yasiharibiwe na kwamba wanyasa wanaamini ukimua ndege huyo
utapata laana.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako