November 15, 2017

HALI YA ZIMBABWE MCHANA HUU



1.Waziri wa Fedha wa Zimbabwe Ignatius Chombo amekamatwa na Jeshi la Zimbabwe. Pia wanajeshi wameua walinzi watatu wa waziri huyo. (Chanzo: PaZimbabwe).
2. Jeshi hilo pia lilitembelea nyumbani kwa Profesa Jonathan Moyo ambaye ni waziri wa elimu ya juu, amekamatwa (Chanzo: NewsDay)
3.Baadhi ya mawaziri wameripotiwa kutoroka, wakiwemo Saviour Kasukuwere  na Makamu wa rais Phelekezela Mphoko anayedaiwa kukimbilia Afrika kusini.

 
4. Waziri wa mambo ya nje, Walter Mzembi amekwenda Zambia kukutana na rais Edgar Lungu kwaajili ya kupata ushauri (Chanzo: PaZimbabwe).
5. taarifa zinasema kuwa kiongozi wa Umoja wa Vijana wa chama cha ZANU-PF, Kudzanai Chipanga ambaye aliitisha mkutano na vyombo vya habari kulipinga Jeshi la nchi hiyo amechukuliwa na Polisi akiwa nyumbani wake mjini Harare (Chanzo: NewsDay).
6. Viongozi watatu wa kundi la G40 linalofanya kazi ndani ya chama cha ZANU-PF na kusababisha migogoro wameripotiwa kukamatwa na Jeshi. G40 ndilo kundi lililosababisha kufukuzwa makamu wa rais, Emmerson Mnangagwa (Chanzo; NewsDay)
7. Wanajeshi wanaulinda pia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Robert Mugabe (Chanzo; NewsDay).
8. Jeshi limedhibiti barabara ya Samora Machel na barabara ya Mtaa wa Sam Nujoma  ambayo inakwenda moja kwa moja hadi nyumbani kwa Robert Mugabe, marufu kwa jina la Munhu Mutapa (Chanzo: NewsDay).

IKUMBUKWE
Mkutano mkuu wa Chama cha ZANU-PF ulitarajiwa kufanyika mwezi Ujao, ambapo pamoja na mengine ungetumika kumchagua Makamu mpya wa rais.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako