April 06, 2008

LINDA Yuko Hoi ,Ligambusa Limemchosha

Ama kweli huu ni urithi kwa Wanyasa.Hivi unakumbuka kisa cha JANETI kutua nyasa na salamu yake "inyahi"?,umesoma au hujasoma?{kitafute humu}.Basi Janeti ana nduguye huyu dada LINDA yaani watoto wa kinyasa hawapotei.Ikawa harusi Jumamosi hii,ngoma za wanaysa zikaporomoshwa hapo,madogoli yakakolea nyuzi bin nyuzi,watu wanakatika viuno kwa maraha ya harusi.Lakini LINDA mtoto wa wanyasa anaishi mjini kakumbana na ngoma za wanyasa "Ligambusa" kaanza kubinua viuno,kafunga kanga kiunoni,viatu kaweka kando,kacheza sambamba na wanyasa,kadhihirisha unyasa licha kuwapo mjini yaani ilikuwa burudani, acha nicheke niringe nina mwanya?.Basi dada kaona ngoja acheze kwa bidii huku mpigaji akivuta nyuzi bin nyuzi Ligambusa linakubali bila ubishi watu wanaselebuka,dada huyu naye kaanza kuonyesha madoido yake ya hapa na pale akamudu kwenda sambamba na watoto wa kinyasa.Kwa hakika ngoma ya Ligambusa kwa wanyasa linachezwa zaidi na vijana kuliko watu wazima kwani inahitaji ukakamavu,mitindo yake ya kasi,inahitaji pumzi.Sasa nashuhudia harusi ya kinyasa hapa nilipo na wanyasa wanasuuza nyoyo za wasio wanyasa, wanaduwaa.Mwishowe ananijia na kuniambia "unalijua Ligambusa mtoto wa nyasa wewe?".kuona hivyo nikamwambia subiri uchovu baada ya kucheza.Mmmh leo jumapili kaamka analamika "Nipo hoi,nguvu sina, mwili umechoka",nikamkumbusha nilivyosema,akabaki kucheka akidai wanyasa ni watu safi sana,yaani licha ya uchovu lakini Ligambusa limenikuna sana natamani kucheza kila siku nyuzi bin nyuzi,kasahau uchovu.Heeeh sijui nimejieleza vizuri kuhusu Linda,hivi inaeleweka?.karibuni nyasa jamani utamu wa Ligambusa mwaujuaaa??

2 comments:

  1. markus mpangala06 April, 2008

    Jamani kuna mtu hapenzi utamaduni wake hapa duniani?Hakika kwa wanyasa mimi nitakufa nikiamini utamaduni huo kwani ndiyo liwazo langu na moyo,najisikia amani sana mambo ya ya wanyasa na kazi zao mza hapa na pale ndiyo maana nikaanza kublogu kwa mtindo wa habari za naysa mahali ambako wamisionari wengi wameishi kwa miaka mingi.Ngoja nitakuja ndogondogo za wamisiaonri wa enzi hizo nikusanye kwanza habri zingine kwani nilizonazo hazitoshi

    ReplyDelete
  2. Hello. This post is likeable, and your blog is very interesting, congratulations :-). I will add in my blogroll =). If possible gives a last there on my blog, it is about the Toner, I hope you enjoy. The address is http://toner-brasil.blogspot.com. A hug.

    ReplyDelete

Maoni yako