April 05, 2008

Wanyasa+Mapenzi+Upendo n.k

Kuna jambo linanikumbusha kitu muhimu sana katika nyanja za uelimishaji kwa wengine.Jambo hili nililitafakari sana katika ulimwengu huu kwani kila siku yanatokea.Mara nyingi nawapenda sana wanyasa wangu kama mfano wa mambo ya hapa na pale.Basi tukio lenyewe lilikuwa nyakati Maalumu zile za wanyasa/Pasaka.Kuna siku tukiwa tunatazama mpira {siyo kwenye Tv}nilipata falsafa ambayo lazima leo niiseme hapa.Ilikuwa hivi; 'Hivi jamani oneni wanaume wanavyopenda mpira wa miguu/soka yaani haielezeki,ndiyo kusema wanapenda mpira kushinda sisi wake zao?Mmh,acheni niseme jamani kama wanaume wote duniani wangewapenda wake zao au kuonyesha mapenzi kwa wake zao kama wanavyoupenda mpira hakika ndoa zingedumu daima.eti nani anabisha hapa?.Oneni wenyewe wanavyokumbatiana kwa upendo wewe unadhani ingelikuwa hivyo kwa wake zao mbona ndoa zingekuwa ni zaidi ya upendo huo?Lakini wao wanakumbatiana sasa wakirudi kwa wake zao wakali,wamefura,wamekunja ndita kwa ghadhabu wala hawawakumbatii,hujifanya hawatuoni vile mmh".
Siyo siri nilijikuta nikiwa na maswali mengi,nikakosa jibu.Kifupi hii ni kauli ya dada mmoja hivi wakati wa kutazama mpira hapa nyasa si unajua siku muhimu kama ile lazima kuwe na burudani kwa wasiokunywa Myakaya,komoni n.k Sasa sijui wenzangu mnasemaje kwani haya ni mawazo ya dada wa kinyasa,analilia upendo wa waume zao mmh sijui wamepeleka wapi,tuusake sasa!

2 comments:

  1. nakubaliana na huyu dada na umwambie hiyo yote yapasa kuwa mvumilivu hivyo ndivyo wanaume wote walivyo. Ndiyo najua sisi wanawake hatuna kitu ambacho tunaweza kusema leo ni lazima nifanye nina maana kuwa nje ya nyumba peke yako hii ni mara chache sana. Sana sana labda kwenda shoping yaani kununua nguo zangu au za watoto. Lakini sio mara zote kwani mume yeye lazima aangalie mpira.

    ReplyDelete
  2. markus mpangala06 April, 2008

    Kuna jambo ambalo naona dadangu analimaanisha kwani kweli ukiwaona wanaume wakiwa na wake zao halafu ukiwatazama katika mambo yanayowahusu wao pekee kama soka utashangaa kuona upendo walionao hakika ni hadithi nzuri.Je wanaume wamepeleka wapi mapenzi kwa wake zao au upendo wao?tuusake sasa

    ReplyDelete

Maoni yako