April 12, 2008

TANGAZO;Nina kila kitu mbona sina Mpenzi?.

Nimekumbuka kisa cha rafiki yangu asimini usiamnini.Yaani leo tangu nimeamka najiuliza hivi kisa hiki hakifai kuwepo hapa?Nikajiuliza vipi kisa hiki watu wakisoma?Lakini nikaona nitakuwa mtu wa visa na vituko lakini sitaacha!...Ni hivi kuna rafiki yangu mmoja hivi anasema anacho kila kitu ambacho mwanamke anaweza kuvutiwa.Ana sura nzuri,ametulia,anajua kupenda,anatabasamu ,mzungumzaji mzuri,anahitaji kupendwa n.k lakini anaseama yeye hajaona mwanamke anayempenda na hajui kwanini.Huyu amekuwa wakati mwingine hana muda wa kukaa na wanawake/wasichana hao anashughulika na kazi zake za hapa na pale.Anashindwa hata kuanzisha mazungumzo na wanawake/wasichana kwani anaona aibu kufanya hivyo na wakati mwingine anaogopa kuwahitaji wanawake/wasichana akidhani watamwona 'mwingi wa habari'.Lakini huyu anamasharti ambayo labda anadhani yanamkosesha wanawake/wasichana.Tatizo lake akianza kuchambua kasoro za wanawake/wasichana anaodhani anawahitaji basi huishia kusema 'mbona huyu anakasoro hii na ile au jambo hili na lile.Yaani yeye kwake kila mwanamke/msichana fulani 'mbona anakasoro hii au ile'.Mpaka naandika nimeshindwa kushauri kwani naona jambo hili lipo mikononi mwake.Je unamtaka na unadhani unaweza kumfariji rafiki yangu huyu?anaumia sana,hajui kwanini hana mpenzi/rafiki wa kike.Mimi sijui cha kumsaidia,karibuni ndani.Yaani yeye kila siku ananimbia "rafiki nina kila kitu mbona sina mpezi?" jamani nifanyeje nashindwa kumsaidia jambo hili.Tangazo

2 comments:

  1. Mapenzi, kama kweli ni kweli ulivyosema ya kwamba huyo rafiki yako ana kila kitu isipokuwa mapenzi. Na pia ana sura nzuri, ametulia anajua kupenda, anatabasamu, mzungumzaji mzuri. Kwa kweli ni ajabu kidogo kama ana sifa hizi zote lakini hakuna mwanamke/msichana anayempenda. Na kama ulivyosema kila msichana/mwanamke anayempata akibahatika basi atatoa kasoro za hapa na pale. Basi ningependa umwambie huyo rafiki yako ya kwamba,kama yeye ana sifa zote hizo hapo juu basi kinachotakiwa atafute msichana ambaye hana sifa kama zake.Pia umesema ana aibu , hii bado sijaelewa kama yeye ni mzungumzaji mzuri kwa nini anaogopa kuwa na mwanamke/msichana. Kama nilivyosema hapo juu mwambie asitafute mwanamke/msichana mzurikwani wote watakuwa wanasema mimi mzuri na mwingine mimi mzuri matokeo yake ndoa/urafiki unakwisha. Au labda yeye yupo kama Bony mwaitege asemavyo anasubiri mungu ampe mke mwema. Kwani hajui binti gani anamfaa.

    ReplyDelete
  2. Mhh! mwambie rafiki yako mapenzi sio kila kitu, penzi ni uamuzi wa mtu. Mapenzi si ya mtu, ni moyo wa mtu, ni kizaa kinene ,ni fumbo kwa wengine. hata kama anaumia na hizo zake hisia.Mwambie huyo rafiki yako Penzi sio pesa, penzi ni uamuzi wa mtu. Mapenzi sio upato kusema tuugawane.

    ReplyDelete

Maoni yako