April 14, 2008

Mitandao Imetekwa Nyara,Kaa Chonjo!!

Nimejikuta nikishindwa kuangua kicheko,yaani nimecheka mpaka jamaa hapa pembeni ninavyoandika akajiuliza hili jamaa vipi?Unajua kwanini?Kipindi hiki hapa nyasa kuna dhoruba kaqli mawimbi yanapiga toka upande wa kaskazini kwenda kusini,basi wanyasa wanaona hii kero,lakini hawajaacha kuvua samaki shauri ni kitoweo chao.Basi jamaa kanishtua hapa nyasa anahisi harufu ya kutekwa nyara mitandao ulimwenguni kwahiyo wanaoblogu na wenye tovuti wawe makini.Nikabisha sikubali bila kuona,lakini nikakumbuka kublogu mpaka niingie mjini Mbinga,Looh! nikakumbuka jambo nililosoma kwa Mwalimu wangu Ndesanjo Macha pale jikomboe.Kumbe jamaa ananishtua hilo wakati nilikuwa nalo kichwani kitambo.Ni Hivi hakika mitandao imetekwa nyara kila anayeblogu akae chonjo saa ya hatari lakini kwa wanyasa tunaweza kujificha ndani ya maji lakini usiulize tutapaje pumzi...sawa..?.Mmmh!!utajuaje kama natania?Jamani mnamkumbuka yule mwizi wa kura za haki kule Kenya?Juzi hapa kateua mawaziri 44 nadhani hii sherehe ya kutafuna mali,basi kateka nyara mtandao; bonyeza hapa http//www.twitter.com/MwaiKibaki,ngoja nisubiri majibu yako..

2 comments:

  1. markus mpangala14 April, 2008

    Jamani Kibaki yupo kwenye mtandao wa twitter hakika dunia ni kama kikombe cha chai kwani kila kona unaweza kuiona ikiwa na chai yake.Mengi utayakuta kwa Ndesanjo Macha hapo JIKOMBOE hebu jaribu bonyeza usome habari nzima

    ReplyDelete
  2. Mmmh nani kasema Kibaki mwizi jamani,huu sasa ni mzaha kwenye mtandao ndiyo maana mnaambiwa nyie wanablogu ni waasi wakubwa wa sekta ya habari mtajiju

    ReplyDelete

Maoni yako