Subi binti Sabato,
Subi binti wa leo,
Subi dada'ngu
wapi mahala pangu;
nianze kulizala wangu,
kulilia wako utaalamu,
nini swahiba wangu,
kimekusibu mwenzangu,
wajua nakudai,
yale maandiko anuai?
ya tiba mwilini,
Subi Kwanza Jamii,
magonjwa ya jamii,
Subi a.k.a Subiraga binti,
u binti safi muwali,
magonjwa tufafanulia,
walai elimu tulijipatia,
vipi Subi a.k.a Subiraga,
mwana wa Iringa ya Ilula?
sijui makwenu wapi,
ila Iringa anuai
NIMEKUMBUKA MAANDIKO YA DADA SUBI SABATO wakati ule pale katika jarida la KWANZA JAMII
nimekumbuka sana, ngoja niingie maktabani nisome maelezo yale. Dada Subi natumaini hujambo.
natamani kuchangia. lakini maneno yangu yataharibu utamu kwa sifa hizi.
ReplyDeletengoja niseme tu, unastahili.
Mmmmh!
ReplyDeleteNi Subi kweli!!
ReplyDeleteHata mimi siongezi kitu!!!
ReplyDeleteMengi uliyo-yanena, mimi nakupa hongera
ReplyDeleteKweli subi ni mwanana, mambo yako si papara.
Upendo kwako bayana,watoa bila kafara
Hongera Subi hongera, mungu akuzidishie
LOOOH, unisamehe mpendwa wangu, rafki yangu Markus. Sikuwa nimeliona toleo hili awali, sasa nimeliona.
ReplyDeleteDah, ama kuhusu swali lako la makala ya afya katika gazeti la KwanzaJamii, ni kwamba, nilikwama kutokana na kuzidiwa shughuli, hivyo ilinisibu kuchagua lipi la kuacha na ndipo ikabidi kuacha hili la makala za KwanzaJamii. Nilifahamu fika kuwa nitakuwa nimewakasoro baadhi ya watu lakini sikuwa na jinsi. Nilishindwa. Nakusihi uniwie radhi wewe na wengineo.
Shukrani kwa maoni yenu nyote mliochangia.