NA MWANDISHI WETU, SONGEA
SASA tunahesabu saa kadhaa
zimebaki kuelekea Tamasha kubwa la aina yake la utalii na uwekezaji katika
wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma .Kulingana na taarifa za uongozi wa wilaya ya
Nyasa tamasha hilo linatarajia kuanza Januari Mosi 2018 na kilele chake ni Januari
6,2018 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim
Majaliwa.
Tamasha hilo ambalo sasa
litakuwa linafanyika kila mwaka limelenga kuvitangaza vivutio vya utalii na
uwekezaji vilivyopo katika wilaya ya Nyasa ili vitambulike na kuvutia
wawekezaji wa ndani na nje.
Tukiendelea kuviibua vivutio
hivyo ni taarifa za uwepo wa dalili za mafuta katika bonde la Ruhuhu.Bonde la
Ruhuhu mwambao mwa ziwa Nyasa Mkoa wa Ruvuma ni miongoni mwa maeneo ambayo
Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) imetaja kuwa yana miamba tabaka
ambayo inaweza kutoa mafuta ya petroli na kwamba utafiti wa kukusanya data
katika bonde hilo bado unaendelea.
Dalili za Kupatikana kwa mafuta Tanzania ni
ishara ya kukua kwa uchumi kimataifa.Kutokana na dalili hizo zinazotia moyo, ni
lazima nchi tajiri zenye Kampuni za kimataifa za utafiti na uchimbaji wa mafuta
zifike katika maeneo yenye dalili za uwepo wa mafuta kama Bonde la Ruhuhu ili
kuhakikisha mafuta hayo yanapatikana.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako