May 31, 2013

MAJIMBO YA UMOJA WA MAJIMBO YA MAREKANI-BARUA


Na Pete Mhunzi, Marekani

Salaam zenu. Mimi kwa jina ninaitwa Pete M. Mhunzi, Mmarekani, Mswahili wa buku. Nilisoma makala yako kuhusu wanasiasa wakiwa pamoja na wajasiriasiasa. Kweli umenena lenye busara kubainisha hulka za viongozi wengi dunia nzima. Nakushukuru.

Madhumuni ya barua hii zaidi ya kupongeza ni kusema machache juu ya neno "jimbo" haswa linalotafsiriwa kwa Kiingereza.  Ulimtaja Rais wetu Barrack Obama katika makala yako kuhusu CUF na kushindwa kwake huko mkoani Tabora. Ulitaja mji wa Honolulu lakini haupo katika Chicago kwa sababu Chicago pia ni mji.  

Honolulu ni mji uliopo kwenye kimojawapo cha visiwa vya Hawaii.  Visiwa hivyo vyote vinatambulika "jimbo".   Chicago ni mji uliopo bara katika jimbo la Illinois.  

Kuna majimbo hamsini katika taifa la Marekani kila moja likiwa na gavana.  Chini ya rais ambaye ana wadhifa ya taifa zima gavana anaongoza serikali ya jimbo ambamo alichaguliwa katika upigaji kura.

Nimeongea kwa upana na urefu juu ya neno hilo "jimbo" pamoja na diwani wa kata ya kati, huko Arusha naye ni mjomba wa mke wangu, kwa jina anaitwa Abdulrasul Tojo.  Tukagundua maana ya "jimbo" katika mfumo  wa siasa za Tanzania ni tofauti sana na maana ya "state" katika mfumo wa siasa za Marekani, yaani taifa la Marekani kwa vile kuna mabara mawili yanayoitwa Marekani.

Tukipima maana kwa ukubwa wa eneo la ardhi la taifa, jimbo hufuata taifa zima halafu ndani ya jimbo kuna "county"  ama  "province" (jimbo la Louisiana peke yake).

Halafu miji ambayo huongozwa na meya anayechaguliwa katika upigaji kura. Bado sielewi vizuri maana ya "jimbo" katika mfumo wa siasa Tanzania!   Nitatia nanga barua hii kwa kushukuru tena mawazo yako ambayo yamenichemshia bongo isitoshe kuridhisha kiu changu cha Kiswahili fasaha.  Asante, asante sana.

Wakatabahu, 
Pete M. Mhunzi
Retired Professor of History
petemhunzi@gmail.com
 

No comments:

Post a Comment

Maoni yako