September 29, 2014

MLO KAMILI NYASA. MASWALI NIYAPATIAYO MAJIBU SASA

Nikiwa mdogo nilikuwa najiuliza sana mafunzo tuliyopewa shuleni kuhusu chakula bora. Nikirejea nyumbani niliona kama hakuna chakula bora na labda tulipaswa kuwa na chakula kingine. Niliona tunanyimwa haki ya chakula bora labda kile kilichoungwa vizuri yaani mboga yenye viungo, mafuta na kadhalika. Lakini jambo moja sikujua ni kwamba kumbe chakula nilichokula kilikuwa bora zaidi.

Vyakula vingi tunavyotumia havina kemikali nyingi bali vyote ni kutoka shambani na kupikwa jikoni. 
Kama samaki basi tunapata moja kwa moja kutoka ziwani na kupelekwa jikoni kwa mapishi. Tofauti na miji mingi ambayo hutegemea samaki kuitoka ziwani lakini hungojea kwa muda mrefu na kumharibu samaki. 
Kwa upande wa Dagaa nayo hali ilikuwa ileile ni ubora wa hali ya juu wa chakula bora.
Vyakula vingi ni vile vinavyotoka shambani moja kwa moja na jambo ambalo linawadia wengi kuwa na afya bora, akili na uwezo wa kufanya kazi nzito. NYASA yetu ni NZURI sana

No comments:

Post a Comment

Maoni yako