February 07, 2018

KUNA HAJA YA KUMSHAMBULIA MFALME WA USWAZI (SWAZILAND) KWA MANENO?


NA KIZITO MPANGALA
KUNA haja ya kupima utaratibu wa maisha yake na maneno aliyolishwa Donald Trump? Ikitokea kwamba mfalme wa Uswazi anahitaji mke mmoja atokee Tanzania, mtajitokeza nafisini hapa?

Mfalme wa Uswazi kuwa na wake wengi ina maana muda mwingi anawaza mapenzi tu kama ashambuliwavyo kwa maneno kutokana na hilo? Kuipima Uswazi na nchi za Ulaya na Muungano wa Mikoa ya Amerika kwamba Uswazi haina maendeleo kama ya nchi hizo kwa kuwa mfalme wake ana wake wengi?


Kwenye maendeleo yaliyo bora zaidi kuliko Uswazi yaani Ulaya na Muungano wa Mikoa ya Amerika wao (wanaume) hawana wanawake? Kipimo cha maendeleo ua Uswazi ni kipi? (Wanajua Waswazi wenyewe) Je, kuna yeyote anakereka na desturi za Uswazi?
Desturi za "INTOBWA" huko kaskazini na kaskazini-magharibi mwa Tanzania hakuna anayekereka nazo? Ila ni desturi za Uswazi tu ndiyo kero? Desturi za kurithi wake kwenye kasri yetu hakuna anayekereka nazo? Lakini desturi za Uswazi tu ndiyo kero? Desturi anazozifuata Jacob Zuma kabilani kwake hakuna anayekereka nazo? Ila ni desturi za Uswazi tu ndiyo kero?

Desturi za kuweka ugoro sehemu za siri huko kanda ya kati kasrini mwetu hakuna anayekereka nazo? Desturi za Uswazi tu ndiyo kero? Desturi mpya ya kuishi bila mke/mume huku mtu ana watoto kila mmoja na baba yake au mama yake kasrini mwetu hakuna anayekereka nazo? Desturi za Uswazi tu ndiyo kero? Desturi za Uarabuni kuwatesa "mabeki tatu" hakuna anayekereka nazo? Desturi za Uswazi tu ndiyo kero?

Desturi ya kuitisha mikutano ya kuombea watu wenye matatizo mbalimbali halafu wakifika eneo la maombi mwombeaji anasema 'wenye shilingi 20,000/= waje mbele nianze kuwaombea, na wenye shilingi 5,000/= bakini kwenye viti hakuna anayekereka nazo? Desturi za Uswazi tu ndiyo kero?

Desturi za kuhadaa watu kwa jina la Mwl. Emmanuel Joseph Masiha (Yesu) hakuna anayekereka nazo? Desturi za Uswazi tu ndiyo kero? Desturi za "undugu, ukabila, ukand" na kadhalik, hakuna anayekereka nazo? Desturi za Uswazi tu ndiyo kero? Kuna yeyote (mwanaume) amefungiwa kuwa na mwanamke? Mfalme wa Uswazi tu ndiye kero?

Kuna yeyote (mwanaume) anayepanga anahita binti asiyeguswa halafu akikosa ailalamikie jamii ya wanawake kwa ujumla kwamba hawajitunzi? Ila mfalme wa Uswazi tu ndiyo kero?

Kuna aliyekereka na desturi ya kusogeza siku mbele ili kutekeleza jambo ambalo lilikuwa linawezekana kutekelezwa siku iliyopangwa bila sababu yenye nguvu? Desturi za Uswazi tu ndiyo kero?

Kuna yeyote anayekereka na desturi ya waendesha pikipiki na bajaji na baadhi ya magari kupita sehemu za waenda kwa miguu? Lakini desturi za Uswazi tu ndiyo kero? Kipimo cha viongozi wa Afrika kutenda vema kiko Ulaya au Muungano wa Mikoa ya Amerika?

Kuna desturi yoyote ya Ulaya au Muungano wa Mikoa ya Amerika ambayo mimi na wewe tumewahi kukereka nayo na ikabadilishwa na kuendeshwa kama mimi na wewe tulivyotaka iwe? Desturi za Uswazi tu ndiyo kero?
Kuna anayekereka na desturi ya "UMBEA" kasrini mwetu? Desturi za Uswazi tu ndiyo kero?

No comments:

Post a Comment

Maoni yako