NA
HONORIUS MPANGALA
©Honorius Mpangala
MAHUSIANO
kuna nyakati yanashindwa kukupa tafsiri iliyo sahihi na ikakuumiza kichwa
kwanini yanatokea unayoyaona. Yawezekana ulikuwa hujui na ukaona wewe ni
mshindi katika haya matukio kumbe unajidanganya.
Kuna
watu katika mahusiano huachana kwasababu ya kimazingira,mawasiliano,imani na
hata kipato. Hawa Mimi nawaweka katika kundi la kuachana kidemokrasia. Kwani
mioyo yao inakuwa bado kwa watu watu wao waliowapenda na huko kwingine waliko
ni kutokana na hizo sababu nilizozisema.
Nianze
na Mazingira, katika Maisha ya kawaida hutoe walioko katika mahusiano huweza
kutenganishwa na mazingira na ikawa moja kwa moja wakaachana. Inatokea mmoja
labda ameenda nje ya nchi au hata nje ya mkoa. Kitendo cha kuwa mbali na
mwenzake kitamfanya aweze kuwa na Wa mazingira aliyopo kwasababu tu mahusiano
yapo popote duniani.
Lakini
katika hilo huenda ikawa kufanya vile ni kujaribu kwenda sawa na mwenendo wa
Maisha kwa mazingira hayo licha ya kwamba uhalisia Wa mapenzi ukawa hauko sana
eneo hilo.Inatokea Mtu anaoa au kuolewa katika mazingira haya. Kitu pekee cha
kuamini ni kwamba kaolewa kwasababu ya mazingira hayo kwasababu kama ni
matibabu ya kihisia yana mtu wake ambaye yeye ndo kila kitu kwake.
Ikitokea
siku akakutana na mtu wake ambaye aliachana nae kimazingira mfano katika maeneo
ambayo mwenzake wake hayupo hakika nakuambia iwe ameoa au ameolewa,jambo la
kwanza itakuwa kurejeshea hisia pale walipoishia kabla ya kupoteana
kimazingira.
Kitakacho
fuata hapo ni kuweka ahadi ya kukutana au ikiwezekana muda huo huo mnara wa
hisia unakuwa unasoma 4G na unakuta watu wanasimamisha shughuli na kutibu hisia
zao ambazo wanajuana kuwa tangu awali hapa ndo ilikuwa mahala sahihi kwake.
Tairi la treni halichengi reli.
Jambo
la kimawasiliano hutokea katika hali ambayo inafanana na. Mazingira. Kwani
yawezekana katika mahusiano mmoja ya wapenzi au wachumba akatoka eneo moja na
kuwa eneo lingine. Sasa kufa kwa mawasiliano kinaweza kusababisha mahusiano
kuvunjika. Lakini kuvunjika huko kunaweza kusababishwa na mawasiliano licha ya
kwamba hao watu wanapendana sana. Baada ya kimya cha muda mrefu hutokea kila
mmoja kubadili maamuzi kutoka hali ya kuzifuata hisia zake kama ilivyo kuwa
awali na kufuata matibabu ya kibiolojia kwa kumpata mtu ambaye atakuwa na
mahusiano ambayo wanafikia kuoana.
Sasa
siku ikatokea hao watu walaiochana kwasababu ya kukosa mawasiliano
,hawakugombana wakaja kukutana katika mazingira ambayo hayakutarajiwa ujue
mshtuko mkubwa utatokea baina yao. Mshtuko huo hauwezi kuzuilika hata kama hawa
watu watakuwa na wenza wao. Kitakacho sababisha mshtuko ni mwili kurejea katika
hisia za kweli juu yao huku akili ikirejea nyuma haraka na kukumbuka yaliyokuwa
yanafanyika katika mahusiano yao.
Hapo
hata iweje kila mmoja atakuwa na lawama juu ya mwenzake. Huku wakiambizana
nimeoa au nimeolewa. Lakini akili nyingine itawatuma kurejesha kile wakichokuwa
wakikifanya kabla ya kuoa au kuolewa baina yao. Hapo lazima hisia za kweli
zijenge hoja toka mwili wa mmoja kwenda kwa mwingine. Hapo ndipo utakapojua
kuwa watu wameoa wake wasio wanawake zao,na wanawake waneolewa na waume wasio
wanaume zao.
Hisia
na mapenzi ya kweli hayawezi kuifanya dini ikashinda katika mahitaji ya watu
wenye mahusiano ya kweli. Kinachofanyika ni kuilazimisha akili ikubali kuwa
dini imepelekea mahusiano kuvunjika na hawa watu kila mmoja akachukua njia yake
kuanzisha mahusiano mengine.
Hapo
tunajidanganya kwasababu hisia hazijawahi kushindwa mbele ya kile ambacho moja
kwa moja kipo katika mwili au mtazamo wa mhusika. Itatokea mwanaume ataweza
kuoa mwanamke kutokana na inani ya dini yake huku yule wa hisia zake akamua
kukubali kuachanae hapo imetumika demokrasia ambayo imesababishwa na imani.
Hata
kwa mwanamke pia kutokana na msukumo wa watu wa karibu ataikubalia akili yake
kuwa ataolewa na mtu mwingine tofauti na yule wa hisia zake ambaye aliziteka na
kumfanya awe mfuasi kamili wa mahusiano. Lakini dini inaingilia na kutenganisha
hili.
Huyo
mtu atakayeo oa au kuolewa naye itakuja siku ataonekans kama ni kituko kwa
mwenzake. Hali hiyo itafanya nafasi ikipatikana hawa wapenzi wenye hisia za
kweli katika mahusiano yao wakakutana iwe Stand ya bus,bandarini,sokoni hakika
nakuambia lazima fikra za 'kuboost' zitawajia tu. Hii ni kutokana na kuachana
kwao ni kwa kidemokrasia hivyo hawana ugomvi wowote hivyo kuifanya paredi
ichangamke ni jambo la kawaida kwao.
Hakika
watatibu hisia zao kwasababu ya akili yao imereje katika wakati ambao matibabu
yake yalikuwa muruwa na hakukuwa na msongo wowote utokanao na uhalisia wa
mapenzi yao.Wataendelea kuibana kwasababu ya hisia zao zimepelekwa kwa watu
ambao ni imani tu imesababisha.
Kipato
nacho ndo jambo kubwa sana ambalo limetamalaki katika Maisha ya sasa.Watu
hujaribu juzilazimisha hisia ziende sehemu ambayo ina kipato lakini kumbe
uhalisia hauko hivyo. Kwani hisia hazitambui kipato zenyewe zinatazama namna
ambayo huweza kumalizwa vyema na kumfanya mtu awe mwenye afya kiakili na
kimaamuzi.
Iko
wazi utatuzi wa mambo atakao ufanya mtu aliyetoka kufanya mapenzi muda sio
mrefu na ule wa yule ambaye hajafanya kwa kipindi utatofautiana. Inasemekana
aliyetoka kufanya mapenzi anakuwa na utulivu mkubwa sana wa kiakili kwa wakati
huo. Sababu kubwa ni kutokana na hisia kupata chakula cha kweli. Hii sawa na
kitendo cha 'reboot' au 'back up' simu yako. Hivyo mtu akishafanya tendo hilo
anakuwa kama ame reboot mwili na kuufanya unakuwa mwepesi wa kila kitu akili na
mwili pia.
Sasa
watu walioshindwa kufikia malengo yao sababu tu kipato ambacho kimesababishwa
na pengine wazazi au wao wenyewe. Hakika kama watakuwa waliachana kidemokrasia
basi hisia huwa hazijifichi. Ni Mara nyingi tunaona wanaume wakubwa wenye kazi
nzuri mke ana kazi nzuri lakini huenda akawa na mwanamke mwingine ambaye hana
chochote kile na wakawaida kabisa. Hizo hisia tena unaweza kukuta mwanamke Huyo
alipikuliwa na mke wa Huyo mwanaume hivyo katika kuheshimu hisia unakuta bado
wanakuwa na mahusiano.
Wako
wanawake ambai licha ya kuolewa na wanaume wenye kipato lakini bado wale ambao
ndo hisia zao ziliko wataendelea kuwaweka katika kumbukumbu za akili zao. Mara
waonanapo basi mzuka na hisia vinatanguzana pamoja. Hii inatokana na kushindwa
kuzuia hisia zao ambazo zilijengeka tangu awali katika mahusiano yao.
Ukitaka
kujua Watu wameoa au kuolewa na wanaume au wanawake wasio wake au Waume zao ni
katika hili. Mara nyingi inapotokea mwanamke akiomba ruhusa ya kwenda kusalimia
wazazi nyumbani kwao Onyo la mwanaume kwa mkewe ni "sasa ndo ukakutane na
tuwanaume twako twa zamani eee" hapo utajua Kumbe akilini anajua kuwa wako
wanaume wa zamani ambao waliteka hisia za mkewa kabla yake.
Ikitokea
mwanaume ndiye anayeenda kusalimia nyumbani kwao utasikia mwanamke anasema
" sasa huko ndo ukaonane na tuwanamke twako twazamani,nakuambia
tutagombana". Kumbe akilini hili lipo na wanatambua kuwa wapo ambao
waliifanya akili ya mume au mke kujisikia amani na faraja kabla tangu. Ndio
maana makalipio kama haya yanatokea ili kulinda hisia zisiweze kuishinda akili.
Wanaochana
kidemokrasia suala la 'reboot' huenda lisiepukike kwasababu asilimia ya
mahusiano yanayokufa moja kwa moja kuanzia akili hadi hisia ni Yale
yalisababishwa na ugomvi baina ya pande mbili.
©Honorius Mpangala
No comments:
Post a Comment
Maoni yako