February 08, 2018

WACHEZAJI WANAVUMILIA MENGI YA MASHABIKI ILA NYOSO KATUONYESHA MOYO WAKE.

NA. HONORIUS MPANGALA
Moyo umeundwa na nyama pamoja na mishipa mingi inayofanya kazi ya kusukuma damu Kwa pande zote.Ni moyo huu huu ambao wengi husema unawauma baada ya kuwasibu mambo ambayo hawata furahishwa nayo. Ni moyo pia ambao humfanya mtu akajisikia amani na furaha baada kuona moyo umeridhika na kufurahishwa na jambo fulani.

Katika Maisha ya kawaida kumekuwa na maneno chungu nzima yanayoweza kuhusisha moyo.Iko misemo kama 'Nina moyo wa nyama' pia imeibuka mingine ya kusema ' moyo sukuma damu sio vingine'. Yote hutokea kwasababu tunajua moyo ndo injini ndogo baada ya ubongo katika kuamua na kuatoa maamuzi ya kuchukizwa au kufurahishwa.Licha ya ubongo kudhibitiambo yote yanayomhusu binadamu lakini moyo niku cha aina yake katika mwili Wa bindamu.  
Tukio alilolifanya Juma Nyoso kwa shabiki wa Simba lina mafunzo pande zote mbili.

Upande Wa kwanza ni Kwa mashabiki Wa soka. Wanatakiwa kutambua wachezaji ni bindamu kama walivyo wao. Kila tendo afanyo mchezaji wakati mwingine hulifanya katika mazingira ya akili ya kawaida kama walivyo binadamu wengine. Ila itashi Wa mashibiki tumefikia hatua ya kuona wachezaji kama kitu Fulani chenye uhitaji tofauti na walivyo binadamu wengine.

Katika mechi ya Real Madrid dhidi ya Depotivo la Coruna nilishuhudia mashabiki wakiwa na vipeperushi vyenye namba saba. Nilipomuuliza mwenzangu akaniambia mashabiki wa Real Madrid wamekuja na ujumbe kwa Ronaldo. Ujumbe unamtaka afunge vinginevyo kocha asimpange. 

Nilishangaa lakini ilibidi niwaelewe tu mashabiki wale kwasababu siku zote wakihitaji jambo lao ni ngumu kuwapinga na ukafanikiwa.Mwanaume akaweka kambani magoli mawili na akaumia vibaya kiasi kwamba hata Mimi niliguswa na moyo kuwa jamaa kawafungia hawa ambao wanamuundia hoja za kipuuzi halafu kaumia hivi. Nafikiri katika mitandao watakuwa wamemuomba radhi Ronaldo.

Shabiki wa Simba aliyepigwa na Nyoso alitakiwa kutambua mtu anayemdhihaki ni nyoso. Na katika hali ya kawaida huyo mtu hana uvumilivu Kwa Yale yanayomgusa moja kwa moja. Kwasababu kuna dhihaka za timu ambazo wachezaji huzibeba Kwa pamoja na kuna zile za kumlenga mtu moja Kwa moja.

Wakati unamuona Nyoso alichokifanya sio ‘fair’ inabidi ujiulize kwanini Hazard alimbutua yule Kijana muokata mipira. Tujiulize ni kipi kilichopelekea Patrice Evra aamue kusitisha mkataba wake na Olympic Marseille, uamuzi Wa kumpiga shabiki je aliambiwa kipi hadi aamue vile. 

Ni Mara ngapi mtu huyo alifanya jambo ka hilo hapo awali. Tujiulize kwanini Eric Cantona aliamua kumpiga yule mshabiki Kong Fu. Tuendelee kujiuliza kwanini Kelvin Prince Boateng kwanini alisusia moja ya mechi akiwa anachezea Ac Milan?

Tuendelee kujiuliza kwanini Sulley Ally Muntari alimua kutoka uwanjani baada ya Ubaguzi aliofanyiwa na mashabiki,moyo wake ulishindwa kipi wakati yeye alikuwa uwanjani.Tujiulize ni kipi kilichowakuta Danny Rose na wachezaji wenzake Wa U 21 kule jamhuri ya Czech hadi wakazua ugomvi katika benchi la ufundi la wapinzani wao.

Twende mbali zaidi kuna sheria gani inayomkuta shabiki moja Kwa moja baada ya kufanyia shambulio la mwili mchezaji au kumtukana. Je ni Mara ngapi matukio ya mashabiki kuwadhihaki wachezaji yameamuliwa katika hali ya kutoa haki Kwa mtendwa?.

Niko upande wa Nyoso hadi sasa Kwa alicho kifanya kwasababu Kuu moja. Mashabiki sana maneno machafu sana Kwa wachezaji na jambo pekee wanalofikiri wao ni sehemu ya kufikisha ujumbe bila kuangalia wanafikisha Kwa mtindo gani. Wachezaji wanavumilia Mengi sana yanayotoka katika midomo ya mashabiki. 

Iliwahi nitokea tukiwa uwanjani nikichezea timu ya watumishi kata ya Chimala dhidi ya Watumishi Wa kata ya Igurusi Kule Mbeya. Nilitukanwa na shabiki tusi ambalo liliumiza moyo wangu nilichofanya ni kumtazama Mwamuzi Wa mchezo nilipooana nafasi ipo ya kumfikishia ujumbe. 

Nilikimbia haraka na kumshambulia Kwa ngumi na mateke na kurejea katika mchezo. Nashukuru sikuonwa na mwamuzi maana nadiliki kusema sikufanya kitendo cha kiungwana lakini pia shabiki hakuwa muungwana kwangu. 

Mioyo ya wachezaji ni nyama kama ilivuo ya wengine.Jambo ambalo mashabiki wanapaswa kujua ni kwamba sio kila neno linamfaa mchezaji yako mengine yanakarahisha mioyo ya watu na mwisho unafikia kupata kama haya.
Upande wa pili wa tukio la Nyoso ni suala ambalo linahitaji elimu ya kutosha sana. Elimu hiyo ni ile Uchezaji Wa kulipwa unatakiwa uwe vipi. 

Uchezaji Wa kulipwa ni mzigo kwelikweli sio masihara. Yako mambo Mengi ambayo unatakiwa kuachana nayo kuwa sehemu ya jamii Kwa kulinda hadhi yako mbele ya jamii.

Lakini unahitaji moyo Wa subira kuweza kuvimudu vitendo vya mashabiki kama hawa wanaopigwa na wachezaji kwasababu hutumia kila aina ya lugha ili kukufanya wewe uwe katika hali isiyo ya kawaida.

Nyoso kama alivyo sio kama kila jambo yeye huwa mchokozi ila kuna hali ya kuchokozwa kwasababu wanamjua kuwa anaumizwa na huwa anafanya tukio katika halo isiyo tarajiwa.

Mi niwaombe tu alichokifanya kinasababu Kwa sababu yeye zio mgonjwa Wa akili hivyo mamlaka zitumie sheria kuliweka sawa jambo hili na Maisha yaendelee. Mashabiki tuwe na akiba ya maneno vinginevyo matukio kama haya yatakuwa Mengi viwanjani.

0628994409

No comments:

Post a Comment

Maoni yako