Na Mwandishi Wetu, Dar es
Salaam
WADAU watano, ikiwamo Kampuni
ya usafirishaji ya Phed Trans inayomilikiwa na mdau wa muziki na kada wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM), Yusuf Mhandeni, maarufu kama (Yusuphed Mhandeni),
wamejitokeza kudhamini Tamasha la Utamaduni linalotarajiwa kufanyika Handeni
mjini, mkoani Tanga, Desemba 14 mwaka huu.
Kambi Mbwana, Mratibu wa tamasha la Handeni |
Akizungumza jana jijini Dar es
Salaam, Mratibu wa Tamasha hilo, Kambi Mbwana, alisema kuwa wadau hao ndio wa
kwanza kujitokeza kuwezesha kwa tukio hilo, huku mazungumzo yakiendelea kwa
wengine wenye nia ya kudhamini tamasha hilo.
Alisema ishara njema imeanza
kujitokeza kuwa wadau na makampuni mengi zaidi yanaweza kuingia kwa ajili ya
kuhakikisha kuwa tamasha hilo linafanyika kwa mara ya kwanza na kuweka historia
katika harakati za kukuza utamaduni kama ishara ya kuleta maendeleo.
“Tunashukuru kwa kampuni hizi
kuwa za kwanza kuthibitisha kushiriki na sisi kwa namna moja ama nyingine juu
ya kufanyika kwa tamasha hili, hivyo naamini kwa pamoja tutafanikisha na
kuwezesha kufanya kile tunachokusudia.
“Bado juhudi zinafanyika
kuingia kwa wadhamini wengi zaidi ikiwa ni njia ya ushirikiano kati yetu
sambamba na wadau hao kuwa na nafasi kubwa ya kutangaza biashara zao kwa
Watanzania wote, hususan wakazi na wananchi wa Handeni kwa ujumla wake,”
alisema Mbwana.
Aidha, Mbwana alitumia fursa
hiyo kuwashukuru walioanza kujitokeza kudhamini tamasha hilo na kuzitakaka
kampuni, taasisi, mashirika mbalimbali pamoja na watu binafsi wenye nia ya
kukuza na kuthamini utamaduni wajitokeze ili kuhakikisha kuwa Tamasha hilo linafanyika
kwa mguso na kufikisha kile kilichokusudiwa kwa hadhira.
Tamasha hilo limeanza kugusa
hisia za watu wengi kutokana na kuwa na mipango thabiti ya kulifanya kwa
mafanikio, ikiwa ni njia pia ya kuwakutanisha wananchi kwa ajili ya
kubadilishana mawazo na kufikiria mambo ya kimaendeleo, huku likiandaliwa na
Raha Company and Entertainment.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako