May 23, 2010

HAPO NDIPO PENYE AKILI,HEKIMA?

"Hapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili na ahesabu ya mnyama huyo, maana ni hesabu ya kibinadamu. Na hesabu yake ni mia sita sitini na sita(666). UFUNUO 13, 18."

Nina hakika msomaji hili siyo jambo geni kwako. Nasadiki kwa dhati kuwa wale waumini wa dini hii wataweza kutupatia tafsiri kamili juu ya mambo hayo, Tunaambiwa 666 ni hesabu ya kibinadamu zaidi na mwenye akili na aihesabu hiyo kama ilivyo katika UFUNUO wa Yohana.

Namba 666 inahusishwa na ishara za siri za aliyekuwa mfalme wa Rumi NERO CALUDIUS CAESAR AUGUSTUS GERMANICUS(37-68). 666 ni tarakimu inayohusishwa na utumwa wa mwanadamu na maangamizi kwake. 666 imetamkwa katika kitabu cha 11 na cha 66 cha Biblia. Cha 11 ni wafalme na cha 66 ni Ufunuo.

Kitabu cha 11 cha Biblia ni 1 wafalme 10; 14, Namba 666 kinasema hivi "Basi uzani wa dhahabu iliyomfikia Suleimani mwaka mmoja ndio talanta mia sita sitini na sita(666). Pia katika kitabu cha Mambo ya nyakati 9;13, ufunuo 13;48. Katika kitabu cha Ezra 2;13 kunatamkwa namba hii 666.

Biblia inavitabu 66 na 666. Hesabu toka Mwanzo hadi ufunuo. Je maana nyingine ufunuo ni mwisho? Ufunuo unafunua nini? Nafsi za Yakobo zilikuwa 666? soma mwanzo 46;26. Kwanini mwanamke wa kiisrael alipangiwa siku 66? soma Mambo ya Walawi 12;5.

Nini maana ya WWW(world wide website)? kwa maana kwa wagiriki W ni sawa na 6 ambayo warumi kwa kirumi ni VI, lakini huita I sawa na 1, V sawa na 5, X sawa na 10 na L ni sawa na 50. Je W ambayo ni 6, inamaana ya 666? Namba hiyo inaleta utata pia katika bunge la ulaya mbona kiti namba 666 hakikaliwi wakati kuna 667 na 665 ambavyo hutumika? Je ni bunge la kishetani ama Biblia iliandaliwa na watu maalumu?

WASHINGTON DOME
ujenzi wake ulikamilika mwaka 1884, una urefu wa futi 555. Ukikokotoa futi 555, utapata inchi 666. Je ni namba 666? Hii inaleta maana gani kwetu na wale waumini wafia dini? Je tunafikiri kwa bidii?

SARAFU YA EURO
Ina nyota 6, fito 6 zimeshika nyota. Julai 20, 1999 bunge la kwanza lilifanyika. Likachagua mwanamke aliyepanda mnyama kama ishara yao. soma UFUNUO 17;3, unaeleza sanamu la mwanamke lililojengwa katika bunge la ulaya mjini Brussels Ubelgiji.

Stemp ya 100 ya EU inafanana na sanamu hiyo. Pia umechorwa katika jengo la Brussels. Hii ni imani gani au ni za mwenyezi mungu? Sarafu mpya ya ulaya ina alama ya mwanamke aliyeketi juu ya mnyama. Je ni maagizo ya mola? Je Yohana anatufunulia mwisho wa dunia au kizazi cha shetani?

Halafu wanazindua biblia yenye lugha 66(?) unajua maana yake katika imani yako? Unadhani Mungu anahuruma sana? Nani alimwumba shetani?
TAFAKARI SANA.

5 comments:

  1. Mtani umenifikirisha sana. Ntaisoma tena na tena hii posti.

    ReplyDelete
  2. Markus kweli wewe ni padiri maana kila nikisoma naona kama nimeelewa nadhani ntafanya kama mtani itabidi niisome tena na tena!!

    ReplyDelete
  3. Mtani, haya mambo wanayachukulia kuwa wako karibu sana na mungu kuliko mungu mwenyewe na wenzao. Watu wandhani kusoma mstari wa imani ya dini ni kujua yale yaliyosababisha dini hizo. Kiabaya zaidi ni kwamba wanasahau hata kujiuliza na ikibidi kumwauliza huyo Mungu. Mtani nakuhakikishia kila jumapili nitakuwa na kitengo cha kukosoa haya mambo. aaaaaaaaaayyyyyyyyaaaaa upo mtani wangu??

    @Da Yasinta wangu samaki na maji, upo? Unajua binadamu wana kawaida ya kujitisha, wanachukulia woga waliojiandalia na kutenda mambo kwa kujilazimisha au kuamini yanatamkwa na biblia. Anguko la kujitisha limekuwa kubwa, tunatakiwa kujiuliza sana na kukokotoa uhalisia wa tafakuri jadidi zetu. Upo Nangonyani wengaaaaa.

    ReplyDelete
  4. Anonymous25 May, 2010

    hakika hapo ndipo penye hekima, panahitaji tafakuri ya kumakinikia haswa,...

    mjadala na uendelee....

    ReplyDelete
  5. Anonymous26 May, 2010

    mmh sijui mwisho wa mambo yote haya ni nini!!!

    ReplyDelete

Maoni yako