May 22, 2010

KWA AFYA YAKO, KARIBU NYASA

Mwili unajengwa kwa matofali? Mchanga unastawisha mwili? Karibu nyasa ujipatie zaidi
Mate yanakutoka kwa HAMU ya kula huu mhindi? Hapo ulipo hakuna mahindi bora? Njoo nyasa ule mahindi yasitegemea mbolea za viwandani, hata mavi ya kuku na binadamu au tuseme mbolea ya SAMADI. Njoo nyasa usipitwe
KARIBUNI NYASA, bwana Matetereka na fmilia mmekula hii kitu? Lol

4 comments:

 1. Unajua mtani huo ni uchokozi hakya nani vile... kitu papaya...hapo hindi bichi. Basi mtani ninapokwenda Mbeya, kitu cha kwanza wanachokifanya nyumbani pale ni kuhakikisha kuna mhindi mbichi ambao huchomwa ili nile.

  Mtani nikiwa Dar huwa sithubutu kula mahindi yale yasiyonoga hadi yawekewe chachandu...

  Ila kutamanisha kiasi hicho siyo vizuri. Ntafanya ziara huko siku moja....Ntakuja na galoni ya ulanzi maana naambiwa huko pombe za kienyeji hazina kiwango.

  ReplyDelete
 2. Hakika huu ni uchokozi usio kifani yaani wewe watu hatujala mahindi tangu miaka... halafu papai sijui mwisho utatutamanisha vindongo au...:-( Markussssssssssssssssss

  ReplyDelete
 3. ha ha ha mtani bwana hakiya nani nakwambia nataka kuhakikisha da Yasinta anaondoka ughaibuni Lol

  ReplyDelete
 4. mambo yenyewe ndio kama haya kwakweli si uongo nitaondoka tu...LOL

  ReplyDelete

Maoni yako