May 26, 2010

WASOMI WETU, WANALILIA UPONYAJI!

Na: Albert Sanga, Tumaini University, Iringa

Nimeamua kuandika makala hii baada ya kutafakari kwa kina swali ambalo liliulizwa na kijana wa kitanzania kupitia katika mtandao wa internet. Kijana huyu anayefahamika kwa jina la Raymond Magambo, ni mwanafunzi wa shahada ya sayansi ya kompyuta Chuo Kikuu Cha Dodoma; anamiliki blogu inayofahamika kwa jina la {raymagambo.blogspot.com}. katika moja ya kurasa za blogu yake ameuliza swali lifuatalo “are the university students in Tanzania well prepared to bring changes in the country? Why?” tafsiri ya Kiswahili ya swali hili ni “Je wanafunzi wa vyuo vikuu katika Tanzania wanaandaliwa vema kuleta mabadiliko nchini? Kwa nini?”.

Kwa bahati nzuri sana ninamfahamu vema huyu kijana Raymond Magambo kwa sababu nilisoma naye kidato cha tano na sita pale Ilboru Sekondari. Ni moja ya vijana ambao wamekuwa na ndoto za kuona wanafanya vitu vya tofauti na vyenye historia za pekee katika dunia hii.

Vijana wa jamii kama ya Raymond Magambo hakika ndio wanaohitajika sana katika kuleta mabadiliko kwa jamii hasa ya kitanzania. Ukiona kijana kama huyu angalau anahoji uthamani na uwezo wa elimu anayoipata basi uwe na uhakika kuwa kuna mambo anatamani yafanyike katika namna fulani ambayo ni nzuri zaidi. Hawa ni watu ambao mimi nawaita “wanamapinduzi wa kutuokoa katika utumwa tuliouridhia”

2 comments:

Maoni yako