July 31, 2010

SIFA ZA WAPUMBAVU NI ZIPI?

Moja ya mambo yanayonisumbua ni wasomi kuendeshwa kiimani na kuondoka katika uhalisia wao(siyo woteeeeeee jamani). Jambo linalonipa shida ni pale ninapomsoma msomi kwa njia ambayo tunaamini anatuelemisha. Kila kona ya dunia unakutaka na sifa ya mtu aitwaye msomi, lakini nimekuwa muumini sana wa jamaa mmoja wa China anayitwa SUN TZU kwanza naamini hakuwa msomi walau kuwa Porofesa aaaahhh samahani Profesa au Mwalimu.... mmmmmh labda nimekosea, waama!

 Kuufikia Uprofesa kuna kanuni zake. Kufikia Udaktari wa Falsafa kuna kanuni zake. Kuufikia sijui utaalamu wa fizikia au kemia kuna kanuni na utaalamu wake. Na je ni nani anaweza kubainisha sifa halisi za Msomi. Na anatumia vigezo gani. Ipo imani ambayo imeenea kidogo kwa baadhi ya watu kwamba ukiwa mjuvi wa vijimambo vingi walau si haba nchini mwetu unaweza kuonekana karaha au kero naam, utakuwa sijui naniiiii

Lakini jambo linalosumbua akili zangu ni kujua kwanini naweza kuishi bila kuwategemea wasomi. Bado najiuliza kwanini Barefoot College kina sifa ambazo wasomi hawatakiwi. Wasomi ni magwiji ni mafundi wa mambo mengi. Lakini sifa hii inaweza kumweka msomi huyu kutojifunza kwa WAPUMBAVU? Na hapo ninajiuliza njia ya kwanza ya kujifunza ni ipi kati ya kuona na kusimuliwa. Maana hata Mpumbavu anaweza kukusimulia na ukaamini na kujifunza.

Naamini labda kinachonisumbua akili yangu ni kutokubaliana na mambo ya kishabiki tu bila kupima na kuamini ndivyo ipasavyo. Ndiyo maana kwa muda mrefu nimetukanwa sana niliposimama na kusema sihitaji kelele kutoka Washington na London ziseme Rais Mugabe ni dikteta na mhuni, nikasema wale waliomwita Mandela gaidi wako wapi, na walipoanza kutengeneza suala hili na kuuvika ulimwengu kuwa dunia inasumbuliwa na ugaidi walidhani sote tuwe watumwa.

Hapana, ndiyo maana nasema endapo suala la kujifunza misemo au kunukuu falsafa za WAPUMBAVU ni UJINGa basi UPUMBAVU na UJINGA wa kwanza utakuwa ni KUZALIWA kwa binadamu maana yapo matendo mengi sana yanayoambatana na BAHATI MBAYA. Lakini kanuni hii inatokana na nini? Na kwanini usipoelewa kitu ukihitimisha haraka bila kujipima umeelewa? Na kwanini usiwekeza kuelewa?               naacha nimetingwa kibingwa......

Basi ni uzembe, basi ni ushabiki ambao sitokuwamo na sitoukubali kwakuwa watu wote wanaamini vuguvugu(kumbuka hawaamini bali wanashabikia kama tupo dimbani). Sifa za wasomi zinajulikana na sifa ya WAPUMBAVU NI ZIPI? Maana kama tunakubali kuwa UJINGA ni jambo baya basi huenda kuamini WASOMI ndiyo wanajua kila kitu ama wao kujiweka katika daraja la juu kwamba wanaweza kufahamu mengi nao ni ubaya zaidi, basi hakuna haja ya kuwepo kwa WAPUMBAVU.

Ninapenda mijadala mitamu inayoumiza kichwa kwa tafakuri hasa pale tunapowaona magwiji wa kufikiri wakijaribu kuibua hisia na hasira za dhahania, kuliko uhalisi. Basi tukishafika hapo tunaweza kujihoji tena kipi kilianza kati ya UPUMBAVU na KUZALIWA? Na kama WAPUMBAVU ni sehemu ambayo mabingwa wa kusoma wanaweza kujifunza kwao, basi hitimisho kwangu halitokwisha kuamini KUNA UHABA WA FALSAFA na labda neno langu baya ni UMASIKINI WA FALSAFA,  Kile unachoamini

Ndiyo, siyo kila FALSAFA inatakiwa kutokana na msomi maana kuna matusi mengine ni FALSAFA. Na siamini falsafa ni zile zitolewazo na wagwiji wake wanaoitwa wasomi ama wale wa kale. Je unaamini nini katika harakati hizi zinazoshabikiwa na watu kama hujapima na kujiridhisha kwamba ndivyo ilivyo? Endapo unajiingiza tu na kudhani ndivyo, basi wewe hustahili kuwepo hapo kwani HUNA FALSAFA, na la zaidi inakata roho na kurudi upya. Je nani anaweza kutupatia SIFA ZA WAPUMBAVU?

Naendelea kutafakari..... nitarudi kinyasa nyasa tu..... najiuliza ZIKO WAPI SIFA ZA WAPUMBAVU

CHANZO;
MARKUS, MWALIMU NYERERE ALIANDALIWA NA NANI?  isome hapa
                   >maoni ya kaka John Mwaipopo na Kaka Matondo

Tujadiliane......................

6 comments:

 1. Wallahi sikujua,
  kama mie ni mpumbavu,
  kama alivyo Markus,
  ambaye pia ni mpumbavu,
  Anapobwabwaja upumbavu,
  wanaosoma pia nao ni wapumbavu,
  Je mpumbavu ni yupi?
  Ni yule anayetoa maoni.
  Yakasomwa na hata wasio wapumbavu,
  Kisha wakaelewa pasipo shaka?
  Au ni yule mwenye nahau?
  Ambazo zimerutubishwa,
  Na nukuu za wapumbavu waliokufa kale?

  nahitaji kujua ni yupi mpumbavu?

  ReplyDelete
 2. mmmmHHHH! mpumbavu! basi hata mimi ni mpumbavu!!

  ReplyDelete
 3. Maisara dadangu, hakika UMENIKUNA SANA KWA TAFAKURI YAKO JADIDI hadi raha
  mimi najiuliza kama wewe
  sifa za wapumbavu ni zipi maana kama kuna watu wanaitwa wapumbavu basi naamini kati yetu kuna wapumbavu. Kwasababu kuu moja, upumbavu ni jambo baya....... haki ya nani najiuliza sijapata jawabu ndiyo maana nasema nahitaji sifa za wapumbavu. Mana suala la in search of identity halihitaji 'link' linahitaji kuelimishwa kwalo. Lakini endapo maoni yanasema kuna nukuu za wafu wa kale hata Yesu ni mfu na ni mpumbavu pia. Na kama tunakubali ndiyo naye yupo hivyo basi sisi ni mazalia ya wapumbavu....... SITUKANI SITANII NAJARIBU KUWAZA TU......... tujadiliane waungwana


  nipo kasi mnooooo


  MZEE WA LUNDUNYASA MWENYEWE

  Markus Mpangala

  ReplyDelete
 4. Mpumbavu??! Unajua niliwaza mbali nikahisi nipo mbele ya mzee wangu anasema `wewe ni mpumbavu, mjinga huna maana' Sasa nasikia hata wanafalsafa ni wapumbavu, kwa vipi?
  Yah, nikakumbuka usemi huo alipenda kuutumia sana baba wa taifa, `upumbavu, mpumbavu...'
  Lakini mimi nataka kukita katika lugha yetu ya Kiswahili, tusije tukaitumbukiza katika tafsiri za watu na kuileta ile maana katika mambo ya kinyume chake. Na ninakubalina na wewe kuwa huku kupenda kunukuu, na hatimaye mtu anapata upro, udo, au whatever, unaweza ukanukuu hata kile unachokiona wewe ni cha kipumbavu lakini `utafanyaje wakati unautaka udo, upro nk.
  Upmbavu ki-kamusi ni ujinga, kutokufanya mambo bila kufikiria, kutokujua nk. Je hawo tunaowanukuu walikuwa `wajinga' walikuwa wamefanya hivyo bila kutafakari.
  Najua ni nini umelenga katika kuuliza hiliswali, lakini mimi nalenga akina sisi ambao tutachukulia hivyo kama ilivyo na mwisho wa siku tutanukuu nakusema wakina nanihii waliandika upumbavu...
  Sasa sifa za wapumbavu ni zipi, kitafsiri ni wale wanaofanya upumbavu, ujinga na mambo yasiyoeleweka katika jamii. JE TULIOWANUKUU WANAZO HIZO SIFA, UJINGA, MMMMH, AAAh, nashindwa kulirudia hil neno manake nakumbuka nilishachapwa kwa kumtusi mwenzangu kwa kumita mpumbavu!

  ReplyDelete
 5. mpumbavu kwani ni nani,
  na hupenda kufikiri nini,
  ana tabia za namna gani,
  hata niweze kumbaini?
  mpumbavu yu na rangi gani,
  hutoa nini mwake mdomoni?
  mimi mpumbavu wa aina gani,
  daraja lipi na lipi kwani,
  maana nami nimo ndani,
  walichosema wao nini nani zaani,
  ama upumbavu ukolee kikombeni.

  nifikiri fikra zenyewe zaani,
  ama nisubiri namshwe kitandani,
  ninayo macho mbona sasa sioni,
  nasimama pembeni ama nipo njiani,
  uoumbavu kwa mwanadamu wataka nini,
  ama wapenda kuvaa mavazi ya aina gani,
  yauzwa wapi sokoni ama gulioni,
  ama yasubiri zama za kampeni,
  wanasema naongea yaliyo pembeni,
  sieleweki sasa kwa sababu gani,
  mwalimu an'toe mi ujinga kichwani,
  hapana mbona ana tongotongo machoni,
  hee! basi makubwa huwezi amini.
  makubwa? kwani yameanza lini?
  kabla hujaja duniani.

  sasa mpumbavu anataka anzuruni,
  ama akajifunze upya ajijue ye ni nani?
  eti sijaeleweka kwa sababu gani?

  ReplyDelete
 6. Je, wewe katika haja ya mkopo haraka ya kulipa bili, upanuzi wa biashara, miili ya ushirika au mkopo binafsi? Wasiliana nasi leo kwa ufanisi na kuaminiwa yako haraka mkopo leo katika kupitia barua pepe: elenanino07@gmail.com

  Regards
  Bi Elena

  ReplyDelete

Maoni yako