January 19, 2009

naona upo karibu yangu

upo karibu au mbali, umewahi kufanya haya tufanyayo? Si mengine ni kuvua tu samaki na kuoposha vindongo hapa nyasa. Karibu nyasa, uwe nasi daima, unatuonaje sasa

6 comments:

  1. Naona niwaonavyo,
    Na hivyo ndivyo mlivyo,
    Ni namna mfanyavyo,
    Na iwe vile iwavyo,
    Nimewaona.

    ReplyDelete
  2. Kaka Mpangala, Yule wa katikati naona kama unafanana nae! Ni mdogo wako nini?

    Hivi nikumbushe ni samaki gani mtaamu kuliko wote anapatikana ziwa nyasa, kuna mwalimu wangu mmoja alikuwa anapenda kumtaja sana, natamani siku moja niende kutalii ziwa nyasa.

    ReplyDelete
  3. Markus, Je unajua kuvua samaki wewe?
    Ahsante kwa picha hii nzuri

    ReplyDelete
  4. aha ha ha ha ha ha ha nacheka sana. jamani haya mambo bwana, blogu raha.

    Fadhy, upo kamili bro, nuf respect

    Keoro: karibu sana nyasa yaani watu watoke Ujerumani hadi kijini kwetu LUNDU na maeneo mengine halafu wewe upo bongo hapahapa unashindwa, nakucheka sana. Hao wadogo nadhani unachokono duh unataka kujua nilivyokuwa navaa mavazi ya kazini au? mmmmhhh we si umezoea jeans,kitopu,shati n.k LAKINI wenzio ndiyo hivyo tena.

    Kaluse): najua unaponiangalia na kuifananisha na kazi unapingana moyoni LAKINI nakwambia hapa sema tu hii kazi ndiyo ilikuwa inanifanya niongeze pesa za matumizi hata nilipoanza kidato! yaani hizi kazi za kuvua zilikuwa nyakati za likizo unafanya kwa kasi mno ili siku ya kuondoka umejaza waleti angalao achulia mbali za wazee wenyewe. natisha aise, labda hujawahi japo kuwa nami beach zetu za fukwe, yaani ni full pumzi

    ReplyDelete
  5. HUJAJIBU SWALI LANGU.........

    ReplyDelete
  6. jawabu ni ndiyo au siyo kiundani pengine inaweza kuambatana na utani. Lakini ndiyo kiundani

    ReplyDelete

Maoni yako