January 21, 2009

nimepoteza ua langu,nalia

Nimepoteza UA nilipendalo, nilisudulo daima. Nimepoteza UA langu kipenzi cha MOYO wangu, upepo wenye nguvu umenipora, wenye harara wamechukua kwa madai nilishindwa kulipenda UA na kulitunza. Najua nalipenda UA langu tena sina mfanowe lakini najuta mimi mwana wa nyasa, mhafidhina, Mnyasa aishie maisha ya kizamani, fikra za kale. Si wajua mahaba ya sasa, uwe kama kumbikumbi, UA langu nalia niwazapo nakonda, sijui nifanye nini waungwana nipeni pole, nishikeni mkono, nitaanguka.

Najua nalia, najua naumia, najua nakonda, najua chakula kibaya kwangu na mwili wangu watetereka, nahojiwa maswali, muungwana kulikoni? Mbona uso umejaa soni kama siyo huzuni? Najuta sana mimi, nalia sana mimi, najua ukimya wangu na mwenendo wangu hauna faida kwa maisha ya kisasa. Kweli nina kasoro zitajwazo, kweli najua ninazo lakini UA langu lijualo limepotea, UA lijualo udhaifu wangu limekwenda mbali nami kwa yule nimjuaye.

Ua langu lijualo kasoro hizo limekwenda ughaibuni, wengine wenye vipawa vya kuonjesha asali za huba wamenyakua bila suluba kwa tiketi ya mateso ili waepukane na maumivu. UA langu linaondoka leo ni siku ya pili, nakiri nilibaini kitambo ila ukimya kwangu silaha, nilijipa moyo licha ya kujua nimebaini. UA langu limetoweka, moyoni nasononeka.

Kwa hali hii, binadamu gani asoweza kurutubisha UA lake alipendalo? Kwanini ujualo ni kosa usilipatie tiba ikiwa yawezekana? Tiba ni kupeperuka, kuniswaga kondeni kwa mafarisayo na wayahudi waua wenzao? Tiba ya kidonda ni kukata mguu au kutibu kidonda, Aaaaaah nakumbuka maeneo ya wahenga, walotujuza kale kwamba ISHI kwaajili yako, furahia maisha yako. UA langu linanipa furaha lakini leo napata simanzi, sioni raha, najua sababu lakini kinywa kinapiga KITE wala AFANALEKI sizihitaji bali nataka UA langu, kikohozi changu. SWALI: Ukiwa na kidonda mguuni unakata MGUU au unatibu kidonda?

Ooooooooooohhhh UA langu limeponyoka, limekwenda mbali limechukuliwa na wenye uwezo wa kushaini HUBA, wenye vipawa vya HAMU. masikini mimi, nalia mwenyewe sina msaidizi UA langu limetoweka. Ukijua una homa, unafanyaje? Utajiua kwakuwa hutaki homa au utapata TIBA? Nakulilia UA langu, rudi kwangu, rudi nyumbani!
Natulia kidogo na wimbo wa IT'S NOT EASY

Jamani ile makala ya 'DINI INAPOTUMIWA KAMA KITEGA UCHUMI' imetoka jana jumanne januari 20./2009 katika gazeti la TAZAMA Tanzania

6 comments:

 1. yo no te entiendo, vos no me entendés pero me encata pasar por acá y ver tus fotos, un gran saludo desde argentina

  ReplyDelete
 2. Ua limekuponyoka, kaka unasikitika,
  Moyo umeshavunjika, imebaki kukuzika,
  Vipi utafarijika?

  Ua limeshatoweka, ua lilothaminika,
  Kamwe halitofutika, moyoni utaliweka,
  Lingali lahitajika.

  Ua limedanganyika, mabaya yatalifika,
  Bora likarekebika.

  ReplyDelete
 3. Mwenzenu mie sijui nisemeje.
  Mbona maua yamejaa na yanauzwa mjini?
  Hebu nenda pale Samora Avenue, maduka ya kuuza maua yamejaa kibao, hela yako tu.

  ReplyDelete
 4. Koero(:
  jamani mbona wanipa simanzi, harara zangu zimalizwe na UA la kununua Samora Avenue? sahau ni UA la moyo, asali wa moyo kama yule wako ushindwaye kwa kikohozi chako, si wajua upendavyo UA lako, maana bila hilo huoni huogi wala husikii la kuambiwa?
  Koero{:
  wajua hilo, wajua UA langu lilivyo kwani ninyi ni aina yenyewe, kwahiyo wajua ninenacho,nimaanishacho. Je umesahau simulizi za LAWINO kuhusu maua ya Samora? UA lako lapendeza ukienda samora?

  Mapenzi kikohozi kujificha huwezi, uzuri wa UA siyo urembo bali tabia, nipe mkono wa pole mwenzio, natetereka na sasa nasafiri kwenda kumpumzika, najipa likizo, akili ipoe, labda UA langu litarudi nyumbani.

  ReplyDelete
 5. Cha muhimu nikujifunza kitu kwa kupoteza!Na kama unaumia uko hai. Na kama uko hai mlango mmoja uliouzoea ukifunga unaweza kustukia milango mingine ambayo ipo na ilikuwepo inayokufikisha kulekule nje.

  ReplyDelete
 6. Kama ni hivyo.
  basi nimeshindwa, naacha!!!

  ReplyDelete

Maoni yako