January 17, 2009

Mseto,Teknolojia na Yasinta+Klayson

Gumzo lilikolea si haba, tukajiburudisha kwa utani wa hapa na pale. Lakini jambo la msingi ni matumizi ya blogu katika kuelemisha na kuwa na marafiki zaidi. Sasa gumzo lilipokolea ilibidi mambo ya teknolojia yaanze kujadiliwa. Mosi ilikuwa huduma poa ya NeoWORX Widgets.
Huduma hii inakuwezesha mambo mengi ikiwemo kujua idadi ya watembeleaji, hali ya hewa, picha na mambo mengine. Hii inamaana pamoja na Free NeoCounter (wageni wanaoitembelea blogu yako), NeoBoard, NeoEarth (hali ya hewa ya mahali unapotaka), NeoPod, NeoFlags( ukipenda bendera mbalimbali ziwepo katika blogu yako), NeoPlanet (mambo ya sayari) na NeoKube.
Huduma hizo ni pamoja na zile za malipo na za bure, sasa kama tunavyojua kwamba blogu zetu zinazidi kupewa kipaumbele kwani zote hizi nia yao ni kuboresha zaidi. Sasa gumzo na mseto wa mazungumzo ilikuwa huduma hizi, lakini binafsi bado najifunza hazijakaa kwenye medulla sawasawa ndiyo maana kuna NeoCounter pekee. Basi bwana Klayson akahoji huduma za bure huzipendi, ikabidi nimweleze mimi bado najifunza hizo kwahiyo polepole.

Mambo ya blogu zetu siku hizi ni mengi huduma ni nyingi mno ambazo Wanablogu inabidi tuzitumie, pia ipo ya Feedbliz , hii ni huduma ambayo kila unachoandika unawatumia wasomaji katika akaunti zao, hivyo wao huingia moja kwa moja kukuta mjadala uliowasilishwa au habari/picha. Hata hivyo ahadi zetu ni kwamba huduma hizi tutaweza kuzitumia iwapo tutajipa muda kuzielewa umuhimu wake. Blogu ni mambo yanayokwenda na mabadiliko sana kwani tayari wataalamu wamebaini siyo upepo wa kupita. Kivumbi cha Gaza blogu zimeweka video, picha na habari motomoto ambazo hutumiwa na mashirika kama BBC, DW, AP, Skynews n.k jamani blogu ni teknolojia ambayo sijui magazeti itakuwaje tuendako maana Thomas Friedman anasemaje katika kitabu chake 'The World is Flat', yanawezekana, AMKA anza WEWE ili tuibadili jamii. Gumzo lilikuwa tamu sana aiseh

No comments:

Post a Comment

Maoni yako