January 12, 2009

nakumbuka sana mambo haya

Huwa nawaona wengi wakiwa katika mazingira haya hapa kwetu nyasa, huwa nakumbuka mengi nikiona namna hii. Nayakumbuka aina ya maisha niliyokulia na kushuhudia mambo haya. Nilidhani ni kawaida lakini siku hizi huwa naumia sana kumbe haikuwa kwaajili yao bali sote bila kujali nasaba zetu. Nawaza sana Lakini sijui jawabu lake labda kuna siku nitawasaidia. Nimeirudisha picha baada ya kujaribu kutafakari ni picha ipi bora kwangu kwa mwaka 2008. Nimeichagua hii nimekulia mazingira ya aina hii hapa kijijini kwetu Lundu maeneo ya nyasa.

8 comments:

  1. Markus umetukumbushia sa hasa MIMI NINAKUMBUKA NYMBA YA BABU YANGU KIZAA MAMA HUKO BUHONGWA MAENEO YA NYEGEZI MWANZA YAANI INAFANANA VILEVILE.

    uMENIFANYA NIMKUMBUKE BABU YANGU JINSI ALIVYOKUWA MPOLE ALIKUWA ANANIAMBIA "MJUKUU WANGU UMEZOEA PWANI HAYA LEO UNALALA NYUMBA YA BABU MVUA IKIJA IKUNYESHEE MPAKA UMUKUMBUKE BABA YAKO SI HATAKI KURUDI TANZANIA MPAKA ATARUDI"

    YAANI NIKIKUMBUKA ENZI HIZO NIKIENDA HUKO NILIKUWA NAPATA RAHA SANA NILIKUWA NAFURAHI KUZIANGALIA NYAMBA ZA AINA HIYO.

    KINGINE KILICHONIFURAHISHA NI KUYAWEZA WAZI MAONO YA KOERO NI NAYE KANIKUMBUSHIA WAANDISHI MAHILI AMBALO WAMESHASAHAULIKA YAANI DUNIA HII INA MAMBO!! YAANI HATA MZEE KATABALO YUKO WAPI MWANDISHI HUYO ALIKUWA ANAPIGANIA LOLIONDO GATE!

    ReplyDelete
  2. sad sad sad!!!!!!!!najitahidi kupata picha halisi,tz kuna madini ya kila aina,utalii lakini wananchi wanazidi kuwa maskini.serikali ikiwa wezesha hawa umaskini utapungua.god bless!

    ReplyDelete
  3. Ukweli picha hii inaelezea maisha wanayoishi asilimia kubwa ya wazalendo.


    Pole sana kwa wazalendo wenzangu amabo "gape" kati ya walio nacho na wasio nacho lizidi kuendelea kwa kasi mpya.

    Ila mimi naamini ipo siku tu..Hata mawe yatasema kama tusiposema.Maana wenye uwezo wa kuongea wamefumba midomo.

    Tutafika tu

    ReplyDelete
  4. Samahani kaka Mpangala, kwenye kompyuta yangu nikifungua blog yako sioni hiyo picha, hata sijui ni kitu gani, na ndio maana nashindwa nichangie nini?

    Unaweza kuniambia labda kompyuta yangu ina mushkeli gani?

    Lakini mbona picha nyingine naziona?

    ReplyDelete
  5. Maisha ni kama nini?
    Nini ni chake kifani?
    Ukumbukapo zamani,
    Huja hisia fulani,
    Za dhati toka moyoni.

    Kumbukumbu za zamani,
    Maisha ya utotoni,
    Hata kama hali duni,
    Usizitupe shimoni,
    Ni muhimu maishani.

    Nimefurahi jamani.

    ReplyDelete
  6. Ni vyema kukumbuka tulikotoka. Kwetu ni kwetu, vyovyote iwavyo.

    ReplyDelete
  7. Nakunukuu''Nayakumbuka aina ya maisha niliyokulia na kushuhudia mambo haya. Nilidhani ni kawaida .....'' Ni kweli kuna maisha ya shida na watu hufikia kuyazoea na kuyaita halihalisi. Ukitoka nje yake ndio unastukia kumbe si kawaida. Nakumbuka nilipokuwa shule ya vidudu Songea ya kikatoliki wakaja masista fulani Wazungu kututembelea na wakashuhudia tukifanya utundu tunafinywa, wacha nao WALIE!Ilinichukua muda mrefu sana kuelewa kwanini mtoto akichapwa au kufinywa iliwaliza hawa masister mpaka nilipo soma saikolojia ya ukuwaji wa mtoto na kugundua utundu mwingi wa mtoto ni ukuaji tu wala hauhitaji achapwe ili aache.

    Nachojaribu kusema ni kwamba labda bado vijijini tunaweza kuipigia kura CCM sio kwakuwa inatusaidia bali ni kwa mazoea na kudhani inabidi na ni kawaida.
    Shida zinazoeleka tusipoangalia hasa kama hakuna kituonyeshacho jinsi ya kujikwamua katika tatizo.
    Maisha Magumu.

    Na ninawasiwasi na mtiririko wa mawazo yangu hapa katika kujaribu kuelezea nikipatacho kwenye picha hii inifikirishayo.
    MAISHA magumu halafu tunakufa!:-(

    ReplyDelete
  8. Watu wangu nashukuru kwa maoni yenu ambayo wakati mwingine yananiliza sana. unaona maoni ya kaka Simon Kitururu? yaani yananifanya nikumbuke maisha yangu yoteeeeee.

    Koero! picha kama hujaiona inamwonysha mama akiwa amebeba mtoto mgongoni na mzigo wa kuni kichwani.
    kama picha haionekani wala usihangaike sana kwani ni suala la mtandao, wakti mwingine kompyuta zinasoma anuani kwa makosa kwahiyo unaweza kukuta inakuletea sura ya ukurasa fulani huku baadhi ya kurusa hazionekani, ni suala la teknolojia- nadhani wataalam zaidi wanajua jambo hilo.

    Wanablogu sote tupo pamoja

    ReplyDelete

Maoni yako