June 12, 2010

MAPENZI NAYO..........

Jamani mnaonaje kuhusu hili nalo??? ,,,,,....... Ngoja unajua nipo kwenye kaofisi kangu hapa??? Unajua mimi huwa sina siku ya mapumziko katika siku 7 za wiki? Labda niamue tu kupumzika, lakini ukweli siku ipo ila sitaki kupumzika..... kwani naamini nitapumzika nikioza nikiwa kaburini... AU?

JAMANI nimekaa hapa nawaza, maana Mtani Fadhy anajua kaofisi kangu kalivyo bwana..... eeeeh  Hapa nawaza eti HAYA MAPENZI inakuwaje mtu unakuwa na muwasho au HISIA za kimapenzi na mtu?? Inakuwaje kwanza mtu ukawa katika hali hii jamani. Nawaza kwasababu unaweza kuwatazama WANAWAKE/WANAUME  wengine yaani unaweza kumwona MWANAMKE/MWANAUME lakini usiwe na hisia naye........ LAKINI kati ya hao anaweza kutokea mtu ambaye WEWE unaamini kuwa UNA HISIA ZA KIMAPENZI KWAKE. Eti jamani mnalionaje hili. Kwanini kwa wengine huna HISIA hizo lakini unazo kwa mtu fulani. Halafu inatokea mtu anaonyesha MAPENZI kwelikweli LAKINI baada ya EMCHEKU anacharuka bin MCHARUKO huyooooooo 'hit and run' AU?

Yaani inamaana hisia hizo ni za kumchungulia mwenzio UVUNGUNI kisha ufute vumbi miguuni utimue zako bila kugeuka nyuma? Najaribu tu kuwaza haya mambo. ETI fikiria kuna watu wanaimbiana NAKUPENDA SANA NAKUPENDA SANA NAKUPENDA SANA lakini baada ya muda HAWATAZAMANI kila mtu kashika hamsa zake huyoooooo tena huko aendako anapata mtu mwingine wimbo uleule NAKUPENDA SANA NAKUPENDA SANA. inakuwaje haya? Ha ha ha ha ha SIJATINGWA ila najaribu kujenga taswira........ ha ha ha Lol..........

Huyu unamwambia NAKUPENDA SANA halafu baada ya miezi au miaka kadhaa upo na mwingine unaimba wimbo uleule NAKUPENDA SANA..... hivi mwisho wake itakuwaje mimi sina jibu sielewi. Hata kama umefunga ndoa lakini mnaachana na wimbo wa NAKUPENDA SANA unahamia kwingine AISEHHHH!!!!!!

Sawa msikose kusikiliza KWAITO, mtafute MANDOZA katika hili bonge la myuziki NKHALAKATA

2 comments:

  1. kuna hadith ninasoma na kuna sehemu inasema "mapenzi yana nguvu kuliko mauti".

    ReplyDelete
  2. Anonymous12 June, 2010

    Mtani unawaza tu hisia za mapenzi....muwazo huo unapata mnogo kama kuna kaulanzi kidogo.
    Fadhy Mtanga.

    ReplyDelete

Maoni yako