June 22, 2010

MIMI NIMEFURAHIA SANA..... VIPI EWE MWENZANGU UNAONAJE HII

Ukisoma blogu ya Mtani wangu Fadhy Mtanga a.k.a Shemeji mtarajiwa, utaelewa kwanini nasema sijatulia. Yeye anatuhabarisha sana kuhusu WOZA 2010 pale Afrika kusini. Sasa na mimi nina jukumu kidogo kuchambua fainali hizi katika tasnia ya habari, ni kazi maalum hii. Halafu jumlisha na shule, jumlsiha na kaofis kangu........ utaona bonge la KUTOTULIA.

LEO nimekuja kiduchu tu.... maana utaanza kuwaza heee mzee wa Lundunyasa imekuwaje kapotea saaaaaannaa. Usijali lakini hata Mama Mchungaji Koero amekuwa Mkulima STADI huko vijijini Miamba n.k.

SASA kuna shairi moja nimelipenda sana, lilitungwa na WILLIAM ERNEST HENLEY wa Uingereza, nimependa mistari hii jamaniiiiiiiiii

"I am the master of my Fate",
"I am the Captain of my soul"

2 comments:

 1. Ahsante kwa taarifa! na uwe na wakati mzuri.

  ReplyDelete
 2. Anonymous22 June, 2010

  shemeji aka mtani (una vyeo vingi kweli) pole sana kwa kutotulia. yaani upo kama mimi. kichwa kimoja mambo milioni kiasi kwamba hata mtani wangu mwingine Yasinta kesha sahau kama nipo duniani maana sionekani.

  mtani eeeh pamoja sana. msalimie.

  fadhy lumuliko mtanga

  ReplyDelete

Maoni yako