February 16, 2009

Kitendawili kimewashinda? Karibuni tule basi!

Nilikuwa nangojea waungwana mjitahidi kufunua bongo zenu, nilidhani kwa wanazuoni kama ninyi lazima jawabu lipatikane ..... lakini wapi bwana, maji yamezidi unga..... yaani tatu bila, tatu bila. Haya basi nimekuja na chakula hiki sijui tutashiba maana samaki mmoja, kwahiyo kula ni kula mbaya kukoimba mboga jamani. Karibuni mkekani, mlozowea mezani msahau kwa leo.

6 comments:

 1. Kaka tutashiba tu hatatukiambulia mfupa umenikumbushia sana hapa chuo cafe zetu bwana kila siku samaki nimeimis sana kahawa ya asubuhi na jioni ya mwananchi nikija dar nitaiparamia we we!!!

  ReplyDelete
 2. "Bwana misosi" itabidi tumwombe Waziri wa Uvuvi na Kitoweo akuajiri kutangaza wizara yake. Ha ha haaaa!

  Unajitahidi kunadi soko la misosi kiasi kwamba kama mtu hujala inakuwa tabu kidogo.

  ReplyDelete
 3. jamani umenitamanisha kweli mmhh nyumbani ni nyumbani tu.tupe basi jibu la kitendawili.

  ReplyDelete
 4. jamani kaka Markus kwakututamanisha hujambo sijui mara ngapi nimeiangalia hii picha na udenda unanidondoka.
  Mary

  ReplyDelete
 5. Ngoja nikafukue kabati nina hakika sikumaliza samaki wangu na huyu nilimnunua baada ya kupata hasira za picha za samaki hapa kwako.
  Umezidi sana kutamanisha, mi nimekutolea uvivu leo hunipati!

  ReplyDelete
 6. kula diyo zangu sana yaani huniambii kitu

  ReplyDelete

Maoni yako