November 24, 2017

JIWE LA POMONDA NA FORODHANI PANAWEZA KUTUPATIA WATU WA 'DIVING' KATIKA MASHINDANO YA OLIMPIKI.

NA HONORIUS MPANGALA

LICHA ya kuwa mazingira mazuri na yenye kila aina ya vivutio lakini wafrika tunashindwa kuwa wabunifu wa katika kuyafanya kama fursa.Mungu aliiumba Afrika hivi ilivyo na kuweka jiografia ambayo nyakati zote watu Wa mataifa ya ulaya wamekuwa wakivutiwa nayo.
Mmmoja wa Warukaji katika Jiwe la Pomonda, Ziwa Nyasa
Iko michezo mingi inayochezwa Ulaya na Amerika inatokana na jinsi wenzetu walivyo makini katika kutumia mazingira yao katika kujipatia fursa ya maisha yao. Nyakati zote mataifa ya wazungu yamekuwa na michezo mingi ambayo ina mashabiki na wanafanya vyema,hakuna michezo ambao unakosa mashabiki Amerika na Ulaya.


Ni huko tunakoona viwanja vya michezo kama ya magongo, tennis, mountain bike, vikiwa na mashabiki kedekede wakishuhudia michezo hiyo ambayo barani Afrika sio rafiki sana. Iko michezo ya kuruka toka juu katika milima,Minara,Madimbwi,Bahari na hata Ziwa. Michezo ile imegawanyika katika nyanja tofauti katika umbali na maeneo ya urukwaji. 


Iko mitindo kama ya   urukaji wa kupatanisha mitindo 'Synchronized Diving' ambo umekuwa maarufu sana katika michuano mbalimbali ya olimpiki. Mitindo huu warukaji huwa wawili wakiwa timu moja na huruka Kwa kufanana mitindo ya urukaji na hauchukui umbali mrefu. Pia kuna ule urukaji wa mitindo wa mbayuwayu ambayo huitwa 'Swallow Diving' hufanyika katika Kwa maeneo yenye umbali wa futi 15 hadi 30. Mrukaji hujitupa tuka eneo la kuanzia kama ni milimani au katika mnara na kuruka kama dege aina ya mbayuwayu. 

Urukaji mwingine ni ule wa kwenye majabali,miteremko mikali iliyoko katika kingo za bahari au ziwa ambao huitwa 'Cliff Diving' mrukaji huachia Kwa umbali wa mita  26 hadi 28 . Aina hii ya urukaji katika michezo hii ya kujirusha ndiyo huwafanya kupatikana warukaji wazuri katika michuano mikubwa ya olimpiki.
CLIFF DIVING
Mfano katika miaka ya 1928 kamati ya olimpiki iliamua kuufanya urukaji wa mitindo ya 'Plain Diving' yaani  urukaji wa maeneo ya uwanda wa pwani na maeneo ya tambarare na ule wa  'Fancy Diving' yaani urukaji wa kibunifu na kufirahisha hadhira uwe kitu kimoja.
PLAIN DIVING
Michezo hii imekuwa maarufu sana katika mataifa ya Ulaya na Amerika tofauti na Afrika. Katika nchi ya Canada kuna shirikisho la kuendesha mashindano ya urukaji kupitia Diving Plangeon Canada DPC. Shirikisho hilo limekuwa likiendesha mashindano hayo mwezi Februari hadi Julai Kwa kuanzia katika majimbo hadi ngazi ha taifa. 

Katika nchi yetu ya Tanzania licha ya kuwa na maeneo mazuri kijiografia lakini tunakosa uwekezaji katika michezo tukihofia mwamko wa mashabiki kutokuwa na mvuto nayo. Hakuna kitu kinachojianzisha chenyewe bali huanzishwa na uvumilivu na kukubali chngamoto ni sehemu ya kufanikiwa.

Katika miteremko mikali ya kitonga katika milima ya Udzungwa ungeweza kusema ndiyo maeneo ambayo wazungu tunawaona wakijiadai nayo Kwa michezo hiyo ya kuruka katika majabali ya milima ya Alps na Himalaya na kuifanya michezo ya ujirushaji kuwa katika ngazi ya kutoa ajira Kwa wanachi wao. Kwa kuanzia sisi kama Tanzania tungeweza kufanya uboreshwaji wa maeneo kama ya Forodhani pale visiwani Zanzibar na Pomonda katika wilaya Nyasa katika kuuhamasisha michezo wa urukaji wa mitindo wa 'Cliff Diving'. 


Ni michezo ambao warukaji huweza kuanzia mita chache na kumalizia katika mita zilizoanishwa kwani watu huruka hadi umbali wa mita 26 hadi 28. Katika eneo la jiwe Pomonda kuna taklibali urefu wa mita 30 na waogeleaji wengi hupenda kuogelea toka nchi kavu hadi lilipo jiwe hilo bila ya kutumia kifaa chochote na hatimaye kupumzika halafu baadae 'Cliff Diving' huanza hapo. 

Inafurahisha kuwatazama warukaji wanaporuka. Sasa katika kuwapatia ajira hapo pangefanyiwa mkakati wa kutengeneza mashindano na mwisho kuwapa warukaji ambao wangeweza kuwakilisha nchi katika michuano mikubwa ya Olimpiki. Kama ilivuokuwa mwanzo mgumu katika kuupenyeza michezo ya urukaji katika Olimpiki ndivyo itakavyokuwa changamoto ya kutooukubalika haraka kutokana na uelewa wa watu.
FANCY DIVING

Eneo la jiwe pomonda limaweza kufumika vyema na warukaji au wakazi wa mwambao wa ziwa Nyasa Kwa kufanya mshindano hata nyakati za mapumziko ya mwaka kama ilivyo Kwa desemba ili kuweka chachu ya kuvutia watu kwenda kupumzika katika fukwe za Liuli ambako jiwe  hilo lipo.

Kila tukionacho kwa wazungu basi tunapaswa kutambua kiliwekezwa na kikavutia mashabiki baada waanzilishi kutokataa tamaa na kuweka malengo mbele. 

Warukaji maarufu wa miruko hiyo huchukuliwa kama watu ambao wejitoa ufahamu kutokana na ugumu wa mazingira lakini sio hivyo kwani kujibiididsha na kuondoa woga ndo mafanikio ya kuweza katika michezo ya ujirushaji. Hii haina utofauti na wale wanajirusha katika majengo marefu ila kinachotofautisha ni maeneo ya kufanyia tukio. Kwa asili ya wakazi wa Nyasa kwao kuruka katika jiwe kama la Pomonda haiwezi kuwa jambo la kuwafikirisha kwani ni michezo ambayo huifanya hata wakiwa wangali wako katika umri mdogo kutokana na malezi ya kimakuzi.

Katika maazimisho ya utalii yanyifanyika kila mwezi desemba mwishoni katika fukwe za Nyasa zingeongeza michezo huu wa kujirusha kwani itaongeza hamasa kwa watalii kutoka pande zote duniani kuja kucheza michezo hiyo hapa nchini. Kama walivyo wao wakiona tu basi hujikuta wakihitaji kutoa mchango wao ili kuboresha mashindano. 
Mazingira tunayo tunachohitaji ni wabunifu wa kuanzisha vitu kama hivi na kusaidia Kwa kiasi kikubwa kuwaepusha vijana ambao wangeweza kuwa washirika na matukio ya unywaji wa pombe au mengine yasiyofaa. Inahitajika mawazo mapya ambayo yatafanya kuinua uwekezaji wa masuala ya utalii kwa ukanda wa kusini hususani fukwe za ziwa Nyasa.

TUWASILIANE: 0628994409

No comments:

Post a Comment

Maoni yako