November 25, 2017

UCHU WA MADARAKA DHIDI YA UZALENDO

KITABU: ZIMBABWE: STRUGGLES-WITHIN-THE-STRUGGLE (1957-1980)”
MWANDISHI: PROFESA MASIPULA SITHOLE
MCHAMBUZI: MARKUS MPANGALA
JESHI la Zimbabwe limetangaza wiki iliyopita kuchukua madaraka nchini humo na kumwondoa Rais Robert Mugabe ambaye ametawala nchi hiyo kwa kipindi cha miaka 38 hadi sasa. Kutokana na hali hiyo tunalaizmika kukumbuka namna mwanazuoni Profesa Masipula Sithole alivyobainisha matatizo ya Zimbabwe kupitia kitabu chake cha “Zimbabwe: Struggles-within-the-struggle (1957-1980)”

Kitabu hiki kilichapishwa rasmi mwaka 1999 na kampuni ya Rujeko Publishers, kikiwa na jumla ya kurasa 230 na kupewa nambari ISBN: 0-7974-1935-7. Profesa Masipula Sithole amewahi kuwa mhadhirti wa Chuo Kikuu cha Zimbabwe na Chuo Kikuu cha Dayton, Ohio, Marekani kwa muda wa miaka minne.

Mwandishi anatuonyesha namna mapambo hayo yalivyoota mizizi na ghadhabu dhidi ya ukoloni lakini yakachipua mapambano mengine baina ya wapigania ukombozi wenyewe.  Matukio yaliyotokea kati ya mwaka 1960 hadi 1980 yanaliachia somo taifa la Zimbabwe na Afrika kwa ujumla wake, kwamba kila zama zinahitaji kuwa na wapigania ukombozi. Kwamba mapambano dhidi ya ukandamizaji hayana kikomo.


Mwandishi anayaangazia zaidi makundi yaliyokuwa yakiongoza mapambano hayo ya kudai uhuru nyakati za ukoloni. Anazungumzia harakati za ZAPU na ZANU, na nyakati fupi za harakati za makundi ya FROLIZI na ANC. 

Makundi hayo yalikuwa yakipambana dhidi ya dui mmoja lakini yakawa yanatumia mbinu tofauti. Wakati fikra za kupambana dhidi ya wakoloni zikipambana moto walijikuta wakiingia kwenye malumbano makali baina yao. Mapambano kati ya ZANU dhidi ya ZAPU, kisha FROLIZI kwa upande wake ikipambana dhidi ya ZANU na ZAPU. 
Nyakati mbalimbali za kihistoria zinathibitisha kuwa wanachama wa chama cha ZANU hawakukubaliana na mbinu walizokuwa wakitumia kupambana dhidi ya kina Lan Smith. Matokeo yake yalizuka mapambano ya wenyewe kwa wenyewe ndani ya ZANU yaliyosababisha maafa na vifo miongoni mwa wapiganaji. Aidha, ni hali hiyo hiyo pia ilijitokeza kwa ZAPU.

Prof. Sitho anasema, “Kifo cha Herbert Chitepo na Josiah Tongogara wa ZANU, pamoja na Alfred Nikita Mangena wa ZAPU vimebaki kuwa kovu na swali lenye utata linalohitaji ufumbuzi kwa muda mrefu sasa, na tuseme kwa wakombozi walio hai au waliotangulia walieleza nini kutokea vifo vya wakombozi hao. Imebaki kuwa siri iliyotundikwa bandarini huku kila moyo wa wana Zimbabwe ukihuzunika na kuksoa majibu, ni nani alihusika kukatisha uhai wa Makamaradi hawa wawili,”?”
Anaendelea, “Kuelezea mapambano ya ukombozi wa taifa ni lazima kuwaangalia waliosimamia na kuongoza mstari wa mbele au nyuma, ilimradi walikuwa sehemu ya vita dhidi ya ukoloni. Makundi ndani ya Zimbabwe hayakuafikiana mbinu sahihi, ni sababu hiyo ikawa rahisi mno kutengana, lakini lilikuwa pigo kwakuwa walikuwa wanapambana dhidi ya adui mmoja,”

Kwenye sura ya 3(uk.34 hadi 43) mwandishi anaeleza kwa kina nini hasa kilitokea hata kusababisha mapambano, visa, uhasama na chuki baina ya ZANU na ZAPU.

Sithole anaeleza, “Mapambano yoyote, uhuru ukiwemo, hatua kwa hatua, mkono kwa mkono, au matumizi ya Kijeshi na kisiasa pia, makundi yote mawili yalikuwa yanatumia mbinu hizo ikiwa na maana ZANU na ZAPU,”
“Kila upande ulinuia kushinda kwa mbinu moja pekee, Kijeshi hali ambayo ingeweza kuwapa ushindi wa kisiasa dhidi ya wakoloni,”


Anatukumbusha kuwa, uteuzi wa mbinu za matumizi ya kijeshi ulikuwa sahihi na ulilenga kubomoa nguvu za jeshi la Lan Smith ambaye alitegemea zaidi uimara wa jeshi kuliko chochote.

Mwandishi anasema kuwa jambo hilo lilisababisha mapambano ya ndani ya makundi, lakini kilichochea zaidi ilikuwa tofauti za kimawazo namna ya kukabiliana na ukandamizaji wa kikoloni.

ZANU kilikuwa na uhusiano na China ambako kilipata msaada wa hali na mali ili kupambana na ZAPU kilichokuwa kikisaidiwa kwa hali na mali na Urusi. Kushamiri tofauti baina ya makundi hayo kulisababishwa na michango mikubwa ya China na Urusi hivyo kudhoofisha mapambano dhidi ya Lan Smith kwa namna moja.

“Mwaka 1963 ZANU/ZAPU vilintwangana vita vya maneno vya namna ya kuanzisha ushirikiano mwingine kwa maslahi ya Zimbabwe, lakini ilikuwa vita binafsi mno na tofauti za kifikra. Kwa upande wao Frolizi walikuwa watata zaidi, lakini walijiandalia mazingira ya kushindwa licha ya kuwa na nguvu zilizowakaribia ZANU na ZAPU. Hata hivyo kuporomoka kwake baadaye hakukusababishwa na Zanu wala Zapu,”

Katika sura ya tano ya kitabu hiki Prof Sithole analeta mjadala mkali kwa kuhoji ni ‘Ni nani alimuua Chitepo”? Mwandishi anachora picha kubwa ya siasa za Zimbabwe. Anaeleza kwa lugha rahisi kuwa Kamati Kuu ya ZANU ilikuwa na mikutano ya kanda, ikiwa ni miaka sita kabla ya kuunda serikali.

ITAENDELEA

No comments:

Post a Comment

Maoni yako