NA MWANDISHI WETU
KAMPUNI ya KAMBAS GROUP yenye
makao yake Makuu jijini Mwanza imeanza kazi ya uchimbaji makaa ya mawe katika
Mgodi Mpya wa Muhukuru wilayani Songea mkoani Ruvuma.
Kwa mujibu wa Afisa Mahusiano
wa Kampuni hiyo, Issa Litunu amesema tayari kampuni hiyo imefungua tawi mjini
Songea ambapo hatua za awali za uchimbaji na usafirishaji zimeanza.
Litunu amesema katika kipindi
cha wiki moja Kampuni hiyo imechimba zaidi ya tani 1000 za makaa ya mawe ambayo
yanasafirishwa kutoka mgodini umbali wa zaidi ya kilometa 100 toka mjini
Songea, yanawekwa eneo la Likuyufusi lililopo Kata ya Lilambo Manispaa ya
Songea kabla ya kusafirishwa kwa wateja jijini Dares Salaam.
Hata hivyo Afisa huyo amesema
kazi rasmi ya uchimbaji inatarajia kufanyika baada ya kupungua mvua za masika
ambazo hivi sasa zinaleta Changamoto ya barabara.Amesema taratibu zote
zimefuatwa kabla ya kuanza kazi ya uchimbaji.Huu ni mgodi wa pili wa makaa ya
mawe katika mkoa wa Ruvuma. Mgodi wa kwanza wa makaa ya mawe ni wa Ngaka uliopo
wilayani Mbinga.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako