March 09, 2010

NIAZIME KONDOMU, NIPO BAGAMOYO

Hakika nakuomba msomaji wangu, watu wangu NIAZIMENI KONDOMU usifanye mchezo nimezidiwa kiasi ambacho inanilazimu kuomba msaada wa kondomu. Haya ni maisha ya huku sasa, maana kila mmoja anafanya kile anavyojisikia, ingawaje ni kawaida sana.

Sasa mimi nasema naomba msaada wa kondomu maana usiku nilivyoupitisha, nimeletewa MAKAHABA wawili, halafu kahaba wa pili akaomba kondomu ili amsadie kahaba mwenzie kwakuwa dume lake halikuwa na kondomu.

Siku zote naamini utafiti wakati mwingine inabidi uingie mwenyewe ushuhudie, na mchakato wangu wa kitabu kile ni lazima niingie maeneo magumu yenye vishawishi adhimu. BASI jana usiku nilikuwa na rafiki zangu, na kwakuwa hawa jamaa wamekuja na Wapennzi wao, wakaanza kunishambulia eti nitajiuuuuu(ulikuwa utani) wakati tukiendelea na porojo akaja mzee wa mapokezi akaniambia 'mjukuu usipate taabu wewe sema tu sasa hivi utapata, huu ni mji wa kimataifa bwana'.

Ikabidi nitulie kisha nikamjibu hebu niletee binti mmoja nimchungulie kidogo. Wakati nipo sehemu ya chakula, chumba changu nimekifunga, kumbe yule mzee akampigia simu kahaba mmoja hivi, nadhani anafahamiana nao. Akajiingiza hapa kwenye nyumba tuliyopo, lakini mlango wangu ukawa umefungwa(sikuwepo).

Punde niliporejea, nikaona mzee ananilaumu mbona binti alikuja, ila ameahidi kuwa atakuja tena. Kweli zilipita dakika 15 hivi, nikiwa chumbani naongea na rafiki zangu, mara mlango ukagongwa na yule mzee, nikawaambia jamani waungwana nendeni chumbani kwenu. Mzee akanikabidhi binti tuelewane......
Akakaa kitini na kuniambia anisikiliza, ikabidi niulize inakuwaje mbona unanijia? Akaniambia kuwa alielezwa na mzee kuwa nahitaji kupunguza ngare.

Nikauliza bei gani bila kondomu na bei gani kwa kondomu. Duh! jamani niazimeni kondomu .......tafadhali sina huku Bagamoyo. Yule binti bila kusita akaniambia kuwa hawezi kulala hapo kwangu kwani mtoto wake yuko nyumbani, kwahiyo bila kondomu 10.000 na tukitumia kondomu 5000.

Upo hapo? nikauliza swali inakuwaje mtoto aachwe nyumbani halafu yeye yuko hapo? Nikajibiwa hayanihusu, bali tufanye kazi(ku*******) kisha atimue zake. Nikatoa amri moja 'nenda kwenu kapumzike na mwanao, siwezi kulala na wewe wakati mwanao yuko mpweke hana mapenzi ya mama. Jamani akaniambia labda sina haja, nataka kumchezea tu kwa muda wake, nikafungua mlango nikamwabia hamna noma wewe nenda tu................

Kumbe yule mzee anakuwa na kigawo chake baada ya shughuli maana alinilalamikia vipi mjukuu unanikosesha kipato? Nikamwambia tafuta mwingine, huyo amezaa kwahiyo mimi na huyo ni mwiko.
Nikaletewa mwingine, huyu ndiye aliniacha hoi kwamba atalala hadi asubuhi hii ninavyoandika hapa, ila suala la kondomu au bila kondomu ni chaguo langu ila bei 10000. Dakika hiyo amekaa kitandani, na mzee ananiambia bei ndiyo hiyo kwahiyo kazi kwako.

Nikasema asante, waweza kwenda binti. Kitu nilichojifunza ni kwamba, niliuliza swali kwa binti huyo na mzee wa mapokezi ni kwanini anadhani kumekuwa na wimbi la ukahaba katika miji mbalimbali duniani? Nilijibiwa ni MAISHA TU. Sijui wewe unayesoma unaelewa nini maana watu wamegeuza miili yao kuwa biashara. Nimejiuliza sana kwanini binti aseme kuwa suala la kondomu ni uamuzi wangu ila anachohitaji ni malipo yake.
Mwenzangu yakanishinda, nikaomba niachwe kama nilivyo... nikawafuata rafiki zangu nikawaambia ipo kazi hapo ni 'cleverness without wisdom'.

KITUKO KIKALI
Mzee wa mapokezi anaye mkewe, lakini siku ya jana amefumaniwa baada ya kuchukua mwanamke mmoja hivi akataka amfi**** unaona yaani nyu***. Sasa alikuwa anataka kumlipa huyo mwanamke 20000 ili afanikiwe kuachiwa nyu****. Lakini ugomvi ukazuka, nyumba nzima zogo, watu wakashituka kuna nini, kumbe jamaa analazimisha ataufune uvungu wa nyuma. Ili kumnusuru ilibidi baadhi wapangaji wamshambulie yule mzee ili kumwachia yule mwanamke, lakini haikuwa hivyo kwani baada ya kuitafuna ile ya kawaida jamaa akawa anataka atafune na nyingine ndogo***.

Mungu wangu makahaba wanaushirikiano, na wanamfahamu mke wa yule mzee ilibidi wachukue hatua za kwenda kumchukua....wakakodi pikipiki(hapa ndiyo usafiri wa haraka sana usiku)..... ili amfumanie mumewe.... halafu kumbe nyumba ndogo naye alikuwa akicheza karibu na sehemu ya tukio ili kujionea...... jamani nipeni kondomu hakika hali hiiiiiiii we acha tu.
Baada ya fumanizi yule mzee kwakuwa alitaka kumfi**** yule kahaba kwani haikuwa siri tena yule mwanamke alikuwa akipayuka na kuwaeleza watu anataka kinyumenyume.....akasimulia yaani jana nimelala saa sita usiku hivi duh!
Sijui nisemeje kwani hii hali inaonekana wazi kuwa inashamiri na sisi wanadamu tunaonekana utashi wetu unadidimia kila kukicha.

Lakini mimi naomba kondomu ili nami nijinufaishe hapa, na rafiki zangu wananicheka sana na kituko changu cha kumkataa kahaba aliyezaa, kisha kumkataa mwingine ambaye baadaye aliomba msaada wa kondomu. Ni mambo juu ya mambo yamenikuna sana, najikuna na kujifunza.......lakini naomba sana mnitumie kondomu maana hapa nilipo sina kwahiyo nahitaji sana msaada wenu waungwana. Karibu Bagamoyo tutalii kwa raha lakini msisahau kuniazima kondomu....

3 comments:

  1. Sababu kubwa ya watu wa Eneo hilo kujiingiza kwenye ukahaba ni "Maisha" kwa mujibu wa ulio wauliza. Ukipata tena fursa ya kuwauliza tena maswali,waulize kama mbali na "ukahaba" maisha hayatakuwepo au kama watashindwa kuendesha maisha yao. Yawezekana watu hawa wanahitaji muongozo fulani ili watambue kuwa hiyo siyo njia pekee ya kujipatia pesa kwani yawezekana kabisa huo ndio ukomo wao wa kufikiri,wanaona ukahaba ndio suluhisho pekee waliloliona. Nitafurahi sana ukiwauliza swali hili na pengine unaweza kuwa mwanzo mzuri wa kuwasaidia kwa wale watakaokuwa tayari.

    ReplyDelete
  2. Mmmmmh tutapona kweli? Eee Mungu tunusuru

    ReplyDelete
  3. Hii makala nzuri sana. Ni kielelezo halisi cha maisha nchini mwetu. Kwa uwazi inathibitisha jinsi mizizi ya uovu mbali mbali, ukiwemo ufisadi, ilivyoenea katika jamii yetu.

    ReplyDelete

Maoni yako