March 10, 2010

KWANINI UMEAMUA KUWA KAHABA? mmh Swali Gumu!

Ni kweli jamani mambo siyo haya tena, na kweli tunatakiwa kuwa makini. Lakini je ni kweli kwamba baadhi wa wanawake wanaamua kuwa makahaba kwasababu gani? Jamani ilibidi niombe radhi baada ya kumhoji binti fulani kwamba kwanini ameamua kuwa kahaba, kwanza alinitazama na kisha akaniuliza shida yako ni kwanini nimekuwa kahaba aua unataka nikupe huduma?

Ni kweli ikabidi niwe mpole, nikatuliza munkari, nikaanza kuongea kirafiki na binti huyo kwani sikuwa peke yangu bali rafiki zangu pia tumejumuika pamoja tunauliza swali hili.
Jawabu la binti huyu ni kwamba 'MAISHA', nikauliza tena je unaifurahia kwakuwa inakuingizia kipato? Nikajibiwa ni swali gumu kulijibu na nisingependa kuongelea hilo.

Nikawa na adabu, nikajaribu kudodosa tena, unajiamini vipi kukubalia kulipwa 10000 bila kutumia kondomu, na 5000 kwa kondomu? Nikajibiwa..... naomba iwe mwisho.... halafu akanitusi mse***** nini,. Ni matumaini yangu hakunilewa lakini baada hakika nakwambia akawa rafiki mwema tu licha ya kazi ya kuuza mwili wake.

Yaani ndani ya nusu saa amehudumia watu wawili wa vyumba tofauti, halafu katika trip hii kuna watu wana wake zao, na wanajivinjari kana kwamba wake zao hawawatoshi, na utadhani hii ni tour ya mwaka mzima wakati ni siku chache tu.

Suala la msingi nimejifunza sana neno 'MAISHA' kwasababu kila unayeongea naye kishkaji anakwambia MAISHA MTU WANGU. Sasa hapo najiuliza tufanye nini ili kuwaondoa watu katika ngome hiyo waliyopo? Sasa kwasababu wanalalamikia kuwa MAISHA, ni wazi hawa ni wahanga wa MAISHA ya kila siku, lakini ni MAISHA gani hayo?

Bila shaka nawe msomaji unaelewa anapokujibu MAISHA, na ikafika mahali kuna binti aliangusha kilio, tukamwomba msamaha, endapo tunamwudhi, lakini hakika nimebaini makahaba hawa kila mmoja analo DUKUDUKU lake, lakini hawajapata mahali sahihi pa kulisema suala hilo. Sijui ni DUKUDUKU gani, na labda ni MAISHA MTU WANGU.
Jamani nipo fasta nabasti kama pancha, sasa tunaenda zetu makumbusho ya watu wa kale hapa. Hii ndiyo BAGA-HEART mji mtamu nimeupenda jamani hadi raha......halafu mmoja akasema... nyie jamaa poa sana, oyaa nitakupeni namba zangu au vipi mkija tena tuwasiliane...... ha ha ha ha nikupe namba msomaji nawe upatiwe HUDUMA? Thubutu.... sikupi ng'ooooooooooooooooooooooooooooooooo, utajijuuuuuuuuuuu

6 comments:

  1. MAISHA, kuna njia nyingi za kutafuta maisha lakini hiyo ya kuuza mwili kwa kweli inasikitisha sana. nakunukuu "Yaani ndani ya nusu saa amehudumia watu wawili wa vyumba tofauti, halafu katika trip hii kuna watu wana wake zao, na wanajivinjari kana kwamba wake zao hawawatoshi, na utadhani hii ni tour ya mwaka mzima wakati ni siku chache tu." mwisho wa kunukuu:- Wanaume wanatafuta nini jamani na sisi wanawake kwanini?

    ReplyDelete
  2. MAISHA BILA IVYO NA MM LEO
    NISINGEKUA HAPA NA NISINGE CHANGIA!!

    NILIPO TOKA NI HUKOHUKOO LKN MUNGU KANI NIJALIA KILAMTU ANA FUNGU LAKE MWIZI PIA!!

    ReplyDelete
  3. Inatia huruma sana hasa kama dada kajiingiza huko kwa sababu ya shida za maisha, sijui na sina uhakika lakini nafikiri kuna njia nyingine mbadala ambazo wangeweza kuzitumia li kujinasua na hii hali ngumu ya maisha

    ReplyDelete
  4. Kaka Bennet nenda ukawaonyeshe hizo njia! jitolee na mungu ata kubariki ktk maisha yako huishi miaka 100

    ReplyDelete
  5. Nice post and this mail helped me alot in my college assignement. Say thank you you as your information.

    ReplyDelete

Maoni yako