KAMPALA, Uganda
VIONGOZI wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki wametia saini kuanzishwa rasmi Baraza la Usalama la
Jumuiya(East African Peace and Security Council) ambalo litashughulikia mambo
mbalimbali ya ulinzi na usalama kwa nchi wanachama wa Afrika Mashariki.
Viongozi hao kutoka
Uganda, Tanzania, Kenya, Rwanda na Burundi wamefikia uamuzi huo juzi jumamosi
wakati wa mkutano wao uliofanyika mjini hapa. Uamuzi wa kuanzisha Baraza la
Usalama la Afrika Mashariki ni kutokana na kitisho cha kusambaa kwa ugaidi kama
ambavyo yalivyotokea Dar es salaam(1998), Nairobi(1998 na 2013), na
Kampala(2010).
Akizungumza mbele ya
viongozi waliohudhuria katika mkutano
Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Richard Sezibera, alisema “Nathibitisha uamuzi
uliofikiwa katika mkutano huu kuanzisha Baraza la amani na Usalama kwa nchi
wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ikiwa na lengo la kuhakikisha ulinzi
na usalama wa eneo hili dhidi ya tishio lolote litakalotokea,”
Wanachama wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki wanakabiliwa na tishio la ugaidi unaofanywa na kundi la Al
Shabab ambalo lina uhusiano na Al Qaeda. Kwenye mkutano huo,
nchi wanachama wamekubaliana kukabiliana na tishio la ugaidi kwa pamoja ili
kuepusha matukio kama yaliyokea mjini Nairobi katika maduka ya Westgate ambapo
zaidi ya watu 60 wasio na hatia walifariki dunia na wengine 175 wakiwa
majaerhu.
Mwaka 2010 kundi la Al
shabab lilidaiwa kufanya mashambulizi katika jiji la Kampala na kusababisha
vifo vya watu 70 baada ya mabomu mawili ya kutegwa ardhi kulipuka.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako