Na Mwandishi Wetu,Mbinga
WAKATI dunia ikiwa
kwenye michakato mbalimbali ya kitaaluma ya elimu, hatimaye kampuni ya
Microsoft Corpoartion imeanzisha Programu mpya ambayo itawawezesha wanafunzi kufanya
mazoezi yote wanayopewa shuleni kupitia
mfumo wa teknolojia mpya.
Kampuni hiyo imebuni
programu mpya ya “Student Advantage” ambayo itawawezesha wanafunzi kupeana kazi
za shuleni,mazoezi ya nyumbani, na masuala yote muhimu ya kitaaluma.
Mpango huo ulitangazwa
juzi, alhamisi na kampuni hiyo wakati ikitambulisha programu ya Microsoft
Office 365 Education ambayo inakadiriwa kutumiwa na zaidi ya wanafunzi milioni
110 wa vyuo , idara na wahadhiri mbalimbali duniani.
Programu ya Microsoft Office
365 Education itawapa fura wanafunzi kutumia kupitia huduma zilizopo mfano
Microsoft Word, OneNote, ambazo zinafanana na huduma za PowerPoint na Excel.
Mpango wa kutumia
programu hiyo unatarajiwa kuanza rasmi desemba 1, mwaka huu huku Vyuo mbalimbali
duniani vikipewa leseni ya Office 365 ProPlus kwa wanafunzi na wahadhiri pamoja
na wakuu wa idara watakuwa wanatumia programu yenye leseni ya Office
Proffessional Plus bila gharama zozote.
Huduma hizo zote
zitawapa nafasi wanafunzi kupata maarifa mbalimbali kupitia Exchange Online,
SharePoint Online na Lync Online, ambazo zipo kwenye programu hiyo ambayo ina
vitu vingine vitakavyomwezesha mwanafunzi kuwasiliana na wengine kwenye vyuo
mbalimbali duniani.
“Wanafunzi watakaotumia
huduma hii kila siku wataweza kufanya akzi zao nyingi za shuleni, na zile
muhimu kwa kutumia programu hiyo mahususi. Hii itawasaidia wanafunzi kuwekana
pamoja katika kazi zao za vyuoni na kuongeza ufanisi wao kitaaluma,” alisema
Mark Chaban, Mkuu wa kampuni hiyo katika nchi za Afrika na Mashariki ya Kati.
Kwa mujibu wa taarifa
ya Microsoft, wamefanikiwa kutembelea vyuo 30 binafsi na vya umma pamoja na
wizara mbalimbali za elimu ili kutoa mafunzo namna ya kutumia programu hiyo.
Alisema mpango huo upo
chini ya Intenational Data Corporation(IDC) ambayo itakuwa ikikusanya taarifa
za maendeleo ya wanafunzi mbalimbali watakaotumia ili waweze kuwa tija katika
soko la ajira na kuboresha maisha yao.
Kampuni hiyo imesema
kuwa inakusudia kufuatilia uwezo wa wanafunzi katika kutumia huduma hiyo,
ambapo watakaoonekana kuwa na kiwango cha juu watachukuliwa na kupelekwa kwenye
makampuni mbalimbali na kulipwa mishahara minono.
Microsoft imepanga
kutengeneza ajira kwa asilimia 28 ifikapo mwaka 2020 ambapo miongoni mwa
wanafunzi milioni 11.5 wataajiriwa kwa vigezo vilivyowekwa.
“Walimu wanapaswa
kubuni njia mpya za kufundisha wanafunzi wao ili kuboresha sekta ya elimu.
Elimu ya mawasiliano ya teknolojia ni muhimu, kwani inarahisisha utendaji wa
kazi, na kuongeza uwezo kwa wanafunzi wote watakaohitimu na kuingia kwenye soko
la ajira sasa na baadaye,” alisema Kunle Awosika, Meneja wa Microsoft nchini
Kenya.
Hatua hiyo imefikiwa
baada ya juhudi za mara wka mara kurahisha shughuli za elimu kwa wanafunzi
ikiwemo tangu kufanikiwa kwa programu ya Microsoft Student 2009 DVD na nyingine
ambazo zimesaidia kuboresha sekta ya elimu na wanafunzi pia.
Student Advantage
inatarajiwa kuwa huduma bora zaidi katika sekta ya elimu na kuwezesha ufanisi
katika sekta hiyo ikiwemo kuwasaidia wanafunzi kuingia katika soko la ajira
wakiwa na weledi wa kuosha.
Makala
haya yameandaliwa kwa msaada wa vyanzo mbalimbali vya mashirika ya habari.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako