Na Mwandishi Wetu, Mbeya
SUALA la elimu ya
mawasiliano kwa umma linazidi kuchukua nafasi kubwa kuliko ilivyokuwa miaka ya
nyuma. Hii inatokana na mabadiliko makubwa ya teknolojia ambayo yamesaidia nchi yetu kunufaika kama
nchi zingine duniani.
Miongoni mwa vituo
vipya vya elimu hapa nchini ni Chuo cha habari cha Digital Media College of
Tanzania, kilichopo katika jiji la Mbeya ambacho kimekuja na mikakati
mbalimbali katika kuitikia wito wa kuboresha elimu ya habari kwa watanzania.
Akizungumza na mtandao huu jijini Mbeya Mkurugenzi wa Chuo hicho, Lucas Kulwa alisema kuwa
mpango wa kuanzishwa chuo hicho ulibuniwa na kampuni ya Radio Consult Limited,
ambayo inaendesha shughuli zake jijini Mbeya.
“Kwa kweli tulifikiria
sana kufanya kitu kwa ajili ya watanzania na nashukuru serikali inatuunga mkono
kwamba sasa hatutategemea waandishi wa habari au wataalamu wa masuala ya
mawasiliano ya umma kusoma fani hiyo hapa Dar es salaam pekee.
“Tumeanzisha chuo hiki
mjini Mbeya na tumeweka makao yetu eneo la Nanenane, sababu tulifanya utafiti
na baadhi ya wataalamu kutoka nje ya nchi ili kujua ni eneo gani sahihi ambalo
litatusaidia kuwafikia watanzania bila kutegemea kitovu cha nchi, yaani Dar es
salaam.
Alipoulizwa na
mwandishi wa makala haya ni kwanini wametumia jina la Digital Media College of
Tanzania, naye alisema, “Kwasasa kuna vyuo vingi sana hapa nchini
vinavyofundisha kozi hizi za media ukiwemo uandishi wa habari na utangazaji,
changamoto kubwa iliyojitokeza ni kwamba wahitimu wote wanaomaliza katika vyuo
mbalimbali wengi wao wanakosa ajira na kibaya zaidi wanashindwa kutumia elimu
yao waliyoipata hata kujiajiri kwa kuandika habari,
Lucas Kulwa, Mkurugenzi wa Chuo cha DMCT, kilichopo jijini Mbeya |
“Pia wanashindwa hata
kumiliki mitandao (websites), kuandika na kuhariri vitabu, kutafuta fursa
mbalimbali kwenye mitandao, kujiunga katika vyama mbalimbali ulimwenguni
vinavyojihusisha na masuala ya uandishi wa habari, kuandaa makala na kushiriki
kwenye mashindao mbalimbali. Kuna mambo mengi sana ambayo mwandishi wa habari
anaweza kuyafanya bila kuajiriwa yaani namaanisha kwa kujiajiri mwenyewe,
“Kwahiyo hii ndiyo
sababu kuu ambayo chuo cetu cha DMCT kinapenda kuiangalia kwamba kwa mwandishi
wa habari yeyote yule kuanzia ngazi ya chini kabisa hadi ya juu wawe na uwezo
wa kujiajiri wenyewe. Kuna tofauti kubwa kati ya nchi yetu na nchi za Afrika
Mashariki na Ulaya kwamba sisi mwandishi wa habari hutegemea ajira tu katika
chombo cha habari na akikosa hapo anarudi kulala nyumbani na kulalamika hakuna
ajira,
“Katika kutafakari ni
kwa njia zipi tutazitumia kumsaidia mwanafunzi au mwandishi wa habari aweze
kujiajiri hata pale anapokosa chombo cha habari cha kufanyia kazi, DMCT tumeona
ni bora tufundishe kozi zifuatazo kwa mwaka 2014:- Certificate in digital
Journalism ya mwaka mmoja, pamoja na Certificate in Radio Production kwa mwaka mmoja.
Anasem,a, “hii kozi ya
Digital Journalism itawawezesha wanafunzi wote kuanza kutengeneza pesa hata
kama ni kiasi kidogo wakiwa wanasoma kutokana na kazi za vitendo watakavyokuwa
wanazifanya, kama kuandika habari na makala na kuziuza katika mitandao
mbalimbali nje na ndani ya nchi.
“Pia watafundishwa
masuala ya kumiliki mitandao (website/blog) kwa undani zaidi hali
itakayowawezesha pia kuendelea kujipatia pesa. Vile vile kozi ya uandaaji wa
vipindi ambayo itatoa waandaji wa vipindi wenye ujuzi wa hali ya juu ambao
wanaweza hata kuuza vipindi vyao kwenye vyombo vya habari mbalimbali.
“Chuo chetu kimepania
kufundisha somo la kompyuta kwa kiwango cha juu zaidi, kwani tumegundua eneo
hili limekuwa kero kwa wanahabari na wananchi wengine watakaopenda kusoma
kompyuta kama nyenzo ya kukabiliana na mabadiliko ya tkenolojia mpya,
“Uwiano wa mafunzo kwa
vitendo, katika chuo chetu cha DMCT tunatarajia kutumia 70% ya mafunzo kwa
vitendo na 30% mafunzo ya nadharia. Tunatarajia kutembelea chombo cha habari
cha nje, kwa kuwa Mbeya ipo karibu na nchi za Malawi na Msumbiji tunatarajia
kufanya mpango wanafunzi wetu wapate nafasi ya kutembelea chombo chochote kikubwa
cha habari nchini Malawi au Msumbiji. Pale DMCT tuna studio ya kisasa
itawasaidia wanafunzi wetu, ndiyo maana tukaanzisha na kozi hii ya Music
Production, TV Production na ICT. Tuna malengo mengi, watanzania watuunge mkono
tu,”
No comments:
Post a Comment
Maoni yako