November 13, 2010

MSWA+NGU= MSWAHILI MZUNGU

 Jamani hili jambo nalifuatilia sana. Na huyu bwana ananifanya wakati mwingine akili iweke kando blogu kwa muda. Pamoja na harakati hizi ninazofanya katika kujikusanyia hata kaelimu ka labda kuwa nitaweza kumpiga mzinga Da Subi au Mtakatifu Kitururu, nimekuwa nikijihusisha sana na suala la lugha ya kiswahili kutokana na maandiko yako mbalimbali.
Basi nimejikuta nifahamiana kidogo na huyu kiumbe hapo pichani anaitwa JASON TAFFS. Huyu ni Rais wa Kiswahili Society pale London katika chuo cha SOAS,  na kwa kiasi fulani anajituma kuwakusanya waungumzaji wa kiswahili kutoka eneo la afrika mashariki pale London. Tayari mkongwe Freddy Macta yuko ndani ya nyumba......... na ujiandae kusoma mahojiano yangu na mzee huyu.
Huyu kijana, tuombe mungu anaweza kuwasili maana wenzake wapo huko Lamu- Kenya ni katika jitihada hizi za kukienzi Kiswahili....
Kiswahili oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
Mungu akijalia najiandaa kufanya naye mahojiano ikishindana basi tena..... shingo pembeni kma nimenyima chakula na Mama Mchungaji Koero binti Mkundi.
Jason Taffs unaweza kutembelea habari zaidi juu ya mradi huo hapa: MSWA+NGU= MSWAHILI MZUNGU

4 comments:

  1. Kiswahili Oyeeeeee!
    Mswangu safi sana, nimependa walivyotohoa maneno hayo mawili na kuyaunga kupata moja linaloleta mantiki. Wakilinyaka hili wanamuziki, basi litasambaa na kuingia katika lugha mara moja.
    Naomba ufanikiwe katika kufanya mahojiano na kaka Jason, nayasubiri kwa hamu kubwa kufahamu wanachokifanya na hatua walioyopiga na malengo yao ya mbeleni kuhusiana na Kiswahili.

    ReplyDelete
  2. mzee wa nyasa pole na jitihada zako za kusaka 'ilmu'. upatapo wasaa wa kuchonga na mzungu mpe maneno kuwa kiswahili cha ukweli kiko bongo na si kenya (ingawaje hizo pande za pate, lamu na mombasa kiswahili kina mashiko kama bongo). tufike pahala tu-udisillusion ulimwengu kuwa tanzania inakitamalaki kiswahili. hii itasaidia watu kama akina CNN na vyuo vya ulaya na marekani kuleta wanafunzi bongo na kuwaajili watanzania. kwa sasa kazi hizi wanapata wakenya simply kwa kuwa wenzetu wana kiherehere cha kujitangaza sana sisi tuking'ang'ania methali 'kibaya chajitembeza, chema ...'imepitwa na wakati.

    ReplyDelete

Maoni yako