November 21, 2010

SITASAHAU ADHABU HII.....

Kwa kweli hii naweza kusema ni adhabu sana lakini nashukuru nimekuwa katika hali ya kawaida sasa. ADHABU yenyewe...... tangu alhamis tarehe 11 mwezi huu nilikuwa na dalili za homa. Lakini dalili zake niligundua mapema kabla ya siku hiyo kwahiyo nilichokuwa nikifanya ni kwenda uwanjani kukimbia sana.

Ilinisaidia lakini ghafla nilitetereka sana kiafya hususani siku hiyo ya alhamis. Ninapochukua uamuzi wa kwenda hospitali ujue nimeshindwa nahitaji tiba. Na ni kipindi kirefu sijaumwa. Jumamosi daktari tarehe 13 daktari akaamua kuniuliza ratiba yangu. Nilipomweleza alishtuka sana.

Kwahiyo ananipa angalizo na usimamizi ukaanza hapohapo;

1. marufu kutumia simu iwe kutuma ujumbe,kupiga au kupokea simu
2. marafuku kutumia kompyuta kwa siku 7 wala huruhusiwi kuisogelea.
3. marafuku kwenda chuoni wala kusoma mada zozote.
4. marufu kwenda kazini kwako kwa siku 7
5. marufu kufanya mazoezi au kutembea kwenda popote.
6. marufu kushika au kusoma kitabu wala gazeti

Nilichoka na nikajua naumwa. Dktari alinieleza nisingekuwa na tabia ya kufanya mazoezi hali yangu ingetetereka zaidi kwani mwili ungelikuwa dhaifu.
Ilinichosha nilidhani niko jela. Nesi akawa anafanya kazi ya kunifanya nijione niko nyumbani. Marafiki waliambiwa wabaki nyumbani kwao wasije kuniona kwasababu natakiwa kupata utulivu.

Hii ilikuwa balaaaaaaaaaaaa jamaniiiiii......... ha ha ha ha sasa nafurahi sanaaaa nimerudi kwa afya njema na mapumziko poa ila natamani kwenda mji wenye hali tofauti ya hewa na hili jiji la pwani la Darichalama. sitasahua adhabu hii mweeeeeeeeeeeeeeee yaani sauti ya kujamba tuuu ndiyo nilikuwa naisikilizia ha ha ha ha ha mcharukoooo paroko.
adhabu hii imekwisha tarehe 21 leo jumapili.

4 comments:

  1. Lakini ingebidi umuulize huyo Daktari kuwa utakula nini ukikaa siku zote 7 bila kujishughulisha, maa inawezena kweli unaumwa lakini kwa mawasiliano ya simu ukapata misaada kutoka kwa wadau mbalimbali

    ReplyDelete

Maoni yako