Na Bahati Chiombe, ARUSHA
WAHENGA walisema kuuliza si ujinga na aghalabu
aulizaye anataka kujua. Wilaya ya Nyasa ni mpya na bila shaka yoyote inahitaji
nguvu za wanyasa wenyewe katika kuleta maendeleo.
Ningependa kuwauliza vijana wanawake kwa waume
mmejiandaa vipi kupokea fursa uwekezaji? Nasaha zangu mjitahidi kuwa waaminifu kwa sababu
Wanyasa waishi mijini watakapoitikia na kuwekeza ktk sekta mbalimbali
UVUVI, KILIMO, UFUGAJI, UJENZI n.k atakuwa anatuma pesa kwa ajili ya mradi
mliokubaliana kwa hiyo inahitajika uaminifu wa kina na taarifa za kweli.
Wengi huzongwa na kazi au shughuli za mijini na muda
wa kuja huko mara kwa mara wanaukosa.Na kama kweli huko Nyasa wengi watakuwa
waaminifu naamini wengi watajitokeza kuwekeza Nyasa na mzunguko wa pesa
utaongezeka na uchumi kukua siku hadi siku.
Osati mtaji ndi faida vhonje vithela kumoa ndi
kumadaba wachikazi asano asano.Zhikom sitimapezane mawa tulo sazino.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako