June 13, 2013

RAIS KIKWETE VS PAUL KAGAME; HAYA NI MAONI YA RAFIKI YANGU BEN SAANANE


Sijutii na sitajutia msimamo huu,ni msimamo wangu Binafsi.Ningekua Amiri Jeshi Mkuu leo hii nisingefanya jambo lingine zaidi ya kum-finance Jenerali Kayumba Nyamwasa kumpindua huyu Bloody Thirsty Dictator Kagame na kule Malawi ningeelekeza Nguvu kwa Prof.Peter Mutharika afutilie Mbali kibaraka mkubwa wa Mabeberu Joyce Banda(shame of Africa) wakati huo huo nikitumia vein tactic ya umuhimu wa Diplomasia

Kagame na Banda wakitaka kujua kuwa Watanzania tunaipenda nchi yetu waendeleze upuuzi waone tutakavyoungana kuwafutilia mbali.Hadi muda huu sijaona kauli kali ya waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe.Kauli za Kagame ni very undiplomatic na huwezi kukurupuka kutoa kauli kama zile wakati Kikwete alikua akiongelea kwa maslahi mapana ya ukanda huu.Pamoja na kuwa Tatizo la Congo Kinshasa,Rwanda na Burundi yana historia ya muda mrefu but there was nothing wrong in JK’s statement.Kenya na Uganda sasa walinywe maana ndiyo walikua makuwadi wa Rwanda katika kuhakisha wanapata admission EAC.Hata katika voting they always votes katika line ya Kenya na Uganda kwa gharama ya Tanzania kama Member State.

Namshangaa Kagame(one of the mastermind of Genocide) kwa kujifanya anayakoromea mataifa ya magharibi kinafiki hasa wanapojadili kuhusika kwake na mauaji ya kimbari,Yeye anawaita kuwa ni wakoloni na huku aki-enjoy matunda ya ukoloni kwa hiyo title aliyo nayo ya Urais.Hajui kwamba kama sio wakoloni waligawa eneo hili leo pengine angekua kama mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo tu maana Rwanda ingekua Mkoa wa Tanganyika hadi leo.

Tanzania tumezungukwa na majirani ambao ni hostile.Yule kibaraka wa kusini Joyce Banda anatia kinyaa,ndiyo maana hata ukanda wa SADC naona heri Bob Mugabe aendelee huko Zimbabwe kuliko Morgan Tsavangirai ambaye angezidi kuimarisha kambi ya vibaraka ukanda wa SADC.Hatuhitaji matusi ya Kagame ndiyo tujue JK ana mapungufu.SisiWatanzania ndiyo tunaojua na ndiyo maana Upinzani tuna hoja ya kutaka JK na Chama chake waondoke madarakani.Tusi la Kagame si kwa JK,ni tusi kwa watanzania wote.By the way,nakipongeza CCM na Kambi Rasmi ya Upinzani kujadili kwa uzalendo above party politics bajeti ya Wizara ya Ulinzi pamoja na kuwa na fungu kubwa.

Pamoja na umaskini wetu,tutumie raslimali zetu vizuri sasa kuimarisha maisha ya Watanzania na kuongeza millitary expenditure na ku-upgrade millitary software na hardware.Tuna majirani ambao wanaelewa lugha ya War Diplomacy zaidi kuliko lugha nyingine.Ukishakia na strong,Modern and formidable Millitary force kwa kawaida ina detterence effects kwa hostile Neighbours bila hata kuingia vitani moja kwa moja….Diplomasia kali inahitajika wakati kama huu.Tuendelee kuliunga Mkono Jeshi letu huko Goma DRC.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako