January 26, 2009

Baridi sana, Nipo Mbeya

Duh! Hii hali bwana we acha tu! Nipo Mbeya jamani, mapumziko ya siku saba hivi lakini naamini kila kitu kinakwenda kama ninavyopanga na ninavyotaka bila kujali ni namna gani nakarahishwa na hii hali. Baridi inanikamata halafu hakuna hata chembe ya faraja, duh! labda kama alivyonipatia wimbo Keoro kuwa niskilize wimbo wa Ziggy Marley.
Jana nilikuwa njiani kuja hapa, mvua, kumbukumbu za maisha yangu ya shule, mitikasi na vioja vya hapa na pale. Mji umekuwa na mabadiliko ambayo naamini kama jiji limepiga hatua kiasi fulani tofauti na mwenendo wa maeneno ya Dar kwenu.
Vipi wanablogu mnaonaje kadiri siku ziendavyo mnafikiria nini kuhusu blogu. Najua wapo wajuaji wa blogu na wale wajuao mchanganuo wa hoja, huku wakipendacho kiwepo ndicho wafanyacho kwakuwa wanajua wafumbacho ni huishia ubongoni mwao! Aiseh!
Tafadhali usiwaaambie uhamiaji kama kesho naingia zangu Malawi kwanza kwa rafiki yangu. Duh! Hii inakuwa ngumu sijui lakini uhamiaji usiwaambie kwani nina kitambulisho cha maktaba tu sina kitu kingine.
Haya, lakini bado nawaza mambo ya mlimani akili imekufa ganzi. Kwaheri kwa leo jamani ila usiwaambie uhamiaji kama kesho navizia kuingia Kalonga kisha ndani ya nchi kabisa.
Pamoja daima! Baridi sana, mapumziko safi-nasonga kwa wajomba unyanjani.

7 comments:

 1. Wakati naandika hapa katika blogu hii pembeni kuna jamaa linaangalia picha za uzinzi, umalaya, na kuchokonoana. Halafu nikimakdilia miaka nampatia kama 35 na kendelea, nashangaa sana. halafu kuna watu zaidi ya wanne wamekaa akatika kompyuta hiyo wakifanya mambo ya ajabu kabisa. tutaandika siku nyingine.

  Alipogundua nimemcheki kafunga ghafla na kuondoka sijui kwenye suluwali kuna kioja au jamaa yake anapinduapindua? nina hasira ndiyo maana nasema ovyo hivi! wizi mtupu/ uzinzi mtupu?

  ReplyDelete
 2. Jamani kitendo cha hao watu kuangalia hizo picha tena hadharani hata mimi kimenikasirisha sana.pole sana kwa baridi kunywa kahawa kwa wingi,huku Canada ndio usiseme kabisa kuna baridi ile mbaya.
  Mary.

  ReplyDelete
 3. Pole kwa yote. Baridi, mipango ya kuzamia na hata huyo mchungulia madubwana.
  Ungemdaka ukamuelimisha. Hujui kishawakimbia mara ngapi na kama hujamrekebisha atarejea na kumkimbia mwingine. Pole sana Kaka

  ReplyDelete
 4. pole sana ila sidhani kuna baridi sana kiasi kwamba unalalamika hivyo.

  ReplyDelete
 5. Markus,

  Si ungenunua Blanket!!!!!?????

  ReplyDelete
 6. Kila la kheri safarini Mkuu!

  ReplyDelete
 7. Mzee wa changamoto! nipo kaka lakini nakiri kosa yule bwana ilibidi kumwelimisha.

  Yasinta) baridi nilipokuwa mbeya ni noma bwana, lakini huku niliko poa tu mambo swadakta kwa mbaaaaali unajiskia utamu utamu

  Koero): mmmmmhhhh umeanza vioja vyako, hilo blanketi si nilikwambia kuwa limeungua moto? Nilikwambia inabidi nianze kutafuta lotto ili nipate sasa wakati naondoka nikajikuta nimesahau lakini usijali najua SOMETHING IS MISSING

  Simon) mkuu nipo kamili kaka usijali sana, naamini itakuwa poa kabisa. Mungu awe nayi daima

  ReplyDelete

Maoni yako