January 24, 2009

ndiyo kazi zetu, ndiyo utamduni wetu

Hii nayo ni kama vile ujuavyo kula na kulala au kupenda na kupendwa. Pengine unajua kuwa tunajua haya mambo. Jamani sijui unawaza nini, au mimi ndiyo nawaza nini. Sijui labda UA alangu, thubutu mmhh pengine. Lakini Koero aliuliza kuhusu picha fulani kuhusu mimi. Eti hii nayo vipi, kweli mimi nipo au? Sijui, lakini haya ndiyo maisha yetu tunatafuta shibe, furaha na pumziko. karibu sana.

5 comments:

  1. Ndugu Mpangala, picha zako ni hazina kubwa. Zinaelezea hali halisi ya huko pande za Ziwa Nyasa. Mimi ni mwalimu na mwandishi wa vitabu, na ninaamini kuwa ukijizatiti utaweza kuandaa kitabu, kikawa na baadhi ya picha hizi na maelezo. Kitabu hiki kitakuwa hazina kubwa ya kutuelimisha sisi Watanzania na wageni pia na kitakuwa hazina kwa upande wa utalii. Fursa ya kukuza utalii pande za Ziwa Nyasa ni kubwa ila bado hatujaifanyia kazi. Wapiga picha kama wewe ni muhimu katika shughuli hii. Nakuachia hilo wazo, na endapo utapenda kulifanyia kazi, nitakuwa tayari kukupa ushauri. Napenda pia kukueleza kuwa picha zako zina mvuto wa pekee kwangu kwa vile nimeshafika mwambao wa Ziwa Nyasa: Mbambabay, Mango, na Nkili. Nakutakia kazi njema.

    ReplyDelete
  2. son fotos my bellas Markus

    ReplyDelete
  3. Nimekupata mzee Mbele, wazo lako ni tamu sana. Kama kuna kiti ninaweza kukizungumzia katika msiaha yangu ni kuandika vitabu, hiki ni kiti nikipendacho, ninachokiona na kukiishi kwa muda mrefu ingawaje nikaamua kublogu. Maisha ya kumbukumbu za nyasa na mwambao kwa ujumla ni funzo kwani kuna utamaduni kati ya nchi zinazopakana katika ziwa nyasa kuwa na historia moja lakini zimemegwa. Hili linaniumiza sana kichwa kwani watu wa malawi, msumbiji na Tz kuna asilimia 95 ya uhusiano mkubwa tokana na mambo yanavyoendelea ukizingatia napenda sana kutafiti mahusiano ya jamii hizi. Hili ni sawa na wasukuma Tz na wazulu wa afrika kusini.
    Nashukuru kwa wazo, tunaweza kulifikia, naamini ipo siku tutafika tu kwa mwendo wa karatasi aua kinyonga tuasonga

    ReplyDelete
  4. nyasa kunaweza kuwa kutamu na baridi ndio maisha yetu hasa walioko kwenye ndoa

    ReplyDelete

Maoni yako