October 14, 2017

HAKUNA WA KUFANANA NA MWALIMU NYERERE

NA MWANDISHI WETU

"Nchi yetu inaongozwa kwa sheria. Hatuwezi kuchagua kiongozi asiyeheshimu sheria akawa anaongoza nchi kwa kushauriwa na mkewe, maana hamjui kesho akiamka atamshauri nini" Mwl. J.K. Nyerere

"Hivyo basi Watanzania watakuwa ni wajinga na mataahira, kama watakubali kuendelea kukandamizwa na watu wachache katika nchi yao wenyewe." Mwl. J.K. Nyerere.
"Hakuna umaskini mbaya kama umaskini wa mawazo, ni umaskini mbaya sana"- Mwl. J.K. Nyerere

"Tatizo la paka kwa panya lingeisha kama paka angefungiwa kengele shingoni: tabu ni kumpata panya wa kuifanya kazi hiyo."- Mwl. J.K. Nyerere
"Mtu aliyejiandikisha kupiga kura, halafu siku ya Uchaguzi haendi kupiga kura, Huyo ni Mpumbavu'' Mwl. J.K. Nyerere

"Dhambi ya ubaguzi ni mbaya sana, sawa na kula nyama ya mtu,dhambi ya ubaguzi haiishi inaendelea tu, leo utabagua kwa kusema sisi ni Wazanzibari hawa ni Watanganyika ,kesho utasema sisi ni Wanzanzibari hawa ni Wazanzibara. Lazima utaendelea, utaona kuna mpemba na Muunguja. Utaendelea tu haiishi sawa na kula nyama ya mtu" Mwl. J.K. Nyerere

"Ukiona mtu anakwambia jambo la kipumbavu na yeye mwenyewe anajua kuwa unajua ni la kipumbavu..ukilikubali ujue amekudharau" Mwl. J.K. Nyerere



"Wakati wa utawala wa awamu ya kwanza si kwamba rushwa haikuwepo, ilikuwepo lakini tulikuwa wakali sana.. Ikithibitika mahakamani kuwa mtu ametoa au kupokea rushwa hatukumuachia hakimu nafasi ya kutoa hukumu peke yake. Tukasema atakwenda ndani kwa miaka miwili na viboko ishirini nanne, kumi na viwili siku anaingia kumi na viwili siku anatoka akamuonyeshe na mkewe" Mwl. J.K. Nyerere

"Mnaingia karne ya 21 mmepanda basi la ukabila, mnaona sifa kuulizana makabila. Mnataka kutambika?!" Mwl. J.K. Nyerere

"Amini nawaambieni enyi Waswahili wachache mnaotawala; mnategemea kweli kuwa mtawaongoza Watanzania kwa lazima wakati wamepoteza matumaini, na mtegemee kuwa watasalia wamekaa kimya kwa amani na utulivu?" Mwl. J.K. Nyerere

"Amani ni zao la matumaini, pindi matumaini yatakapotoweka kutakuwa na vurugu katika jamii." Mwl. J.K. Nyerere

"Nitashangaa kama hawa Watanzania watakataa kuasi. Kwanini wasiasi?" Mwl. J.K. Nyerere

"Wakati wengi wa wananchi wanapopoteza matumaini unajenga volcano. Volcano hii italipuka siku moja. Labda kama watu hawa ni wajinga." Mwl. J.K. Nyerere

"Na hakutakuwa na watu wa kizazi hiki na karne hii ambao watatakiwa kujitoa muhanga kwa ajili ya maisha bora katika siku zijazo wakakubali, wakati wanawaona watu wachache wakiendelea kuneemeka machoni pao bila kujali wakati ujao, wakati wao na watoto wao wakiendelea kuishi katika maisha duni na dhalili." Mwl. J.K. Nyerere

Siku chama kilipokuwa kinamuaga mzee Kawawa (Alipostaafu rasmi siasa za majukwaani) Katika hotuba ya shukrani alisema, pamoja na mambo mengine: ‘ "Naahidi nitakufa nikiwa mwanachama mwaminifu wa CCM"
Ilipofika zamu ya Mwalimu Nyerere kuzungumza, akasema: ‘

"Rashid una roho ngumu. Utakufa mwanachama mwaminifu wa CCM?! Mimi siwezi kuyasema haya. CCM inaweza kubadilika. Siku ikiacha misingi nami naachana nayo kwasababu CCM si mama yangu. Ninaye mama mmoja na siwezi kupata mwingine" Mwl. J.K. Nyerere

"Njia pekee ya kumsaidia masikini ni kumwelimisha mtoto wake". Mwl. J.K. Nyerere

"Siku inakuja ambapo watu watachagua kifo kuliko fedheha na ole wao wale watakoiona siku hiyo! Na ole wao wale watakakaoifanya siku hiyo isiepukike. Natumaini na kusali kuwa siku hiyo kamwe haitofika" - Mwl. J.K. Nyerere (Januari, 1966)

Nukuu nyingi kati ya hizi zimo katika kitabu kinachoitwa : Reflections on leadership in Africa: forty years after independence : essays in honour of Mwalimu Julius K. Nyerere, on the occasion of his 75th birthday ' , by Haroub Othman, VUB University Press, 01 Jul 2000.

No comments:

Post a Comment

Maoni yako