Pichani ni Nyumba ya Mwalimu Nyerere iliyopo eneo la
Magomeni ambayo kwa sasa ni makumbusho ya Taifa.
Mwaka 1957 Mwalimu akiwa anafundisha shule ya Sekondari Pugu
alikusanya mafao yake ya ualimu na akamwomba rafiki yake Mustafa Songambele
amtafutie kiwanja katika maeneo hayo, naye akamtafutia kiwanja hicho kilichopo
Magomeni, Mtaa wa Ifunda.
Enzi hizo Magomeni ndiyo ilikuwa kama Masaki ya sasa na
Mwalimu alitaka kukaa mahali penye mazingira salama na ulinzi ili kuendelea na
harakati za kulikomboa Taifa kutoka kwa Mkoloni wa Kiingereza.
Lakini baadae Mwalimu kwa Moyo wa ajabu akaitoa nyumba yake
mwenyewe aliyoijenga kwa jasho lake na mafao yake na kuikabidhi kwa Serikali ya
Tanzania ili iwe Makumbusho ya Taifa kwa kizazi hiki na vizazi vijavyo
vikumbuke ni wapi tulipotoka na wapi tunaelekea.
Mwalimu wakati wa Uhai wake katika Ngazi ya Familia alikuwa
Baba na Babu pia, angeweza kujilimbikizia yeye na familia yake Mali zote za
Taifa lakini kwake Tanzania na Afrika nzima ilikuwa Zaidi ya Maisha yake
binafsi na Familia.
No comments:
Post a Comment
Maoni yako