October 14, 2017

WATU WASIOJULIKANA WATAIKIMBIZA AFCON U-17 2019

NA HONORIUS MPANGALA 
 
MWANDISHI maafuru wa fasihi kutoka Nigeria,marehemu Chinua Achebe katika kitabu cha 'Things Fall Apart' alisema kukimbia matatizo sio njia sahihi ya kutatua hayo matatizo. Wakati msomaji wa fasihi hiyo akiona kama burudani kusoma vibweka vya Okonkwo lakini kuna mafundisho katika kitabu kile. Nyakati zote huwezi kuona ugumu wa jambo kama halijakutokea.
Chinua ananifanya nihusianishe matukio ya watu wasiojulikana na hatima ya Nchi katika nafasi ya kuandaa fainali za mataifa ya Afrika kwa vijana wa chini ya miaka 17.
Serengeti Boys wakifurahia katika moja ya mabao waliyofunga katika mechi za kimataifa
Ukimya wetu katika kuchukulia kila jambo ni kitu kinachofanyika na tukashindwa kutambua tatizo au kuwabaini wahusika linaweza kutuondolea mwonekano wetu nje ya mipaka ya nchi.

Matatizo yanatakiwa kutatuliwa kwa kufahamu chanzo na kuchukua hatua ya kuyamaliza. Sisi kama Taifa tuna hamu kubwa na kuona tukifanikisha Michezo inafanyika vyema hapa nchini kwa kuhusisha sekta zote kushiriki vyema.
Labda nikumbushe jambo moja baada ya Afrika kusini kutangazwa kama waandaaji wa fainali za kombe la dunia mwaka 2010. 



Moja ya mataifa ambayo yalikuwa na kampeni za kuifanya Afrika kusini kama sio sehemu makini kwa fainali zile ilikuwa ni Hispania. Naweza kusema wahispania ubaguzi ni jambo ambalo watu wamekua nalo wanapenda kujiona bora kuliko wengine.
Kikosi cha Serengeti Boys
Hispania walieleza mengi yaliyohusu Usalama. Na Hayati Mzee Nelson Mandela aliihakikishia FIFA atahakikisha na waafrika kusini watakuwa wenye kutambua thamani ya nafasi waliyopewa kuandaa fainali zile. Wasauzi na waafrila kwa ujumla walichukizwa na maneno yaliyokuws yakitamkwa na Hispania na Mataifa mengine yaliyokuwa nyuma yao.

Walipoenda kucheza Mashindano ya mabara juni 2009,Hispania waliduwazwa na hali ya kiusalama kwa wasauzi maana walionyesha jinsi walivyojipanga. Licha ya kuona hali ile baada ya mashindano yale Hispania waliweza kuja na hoja nyingine mfu kuwa FIFA wakataze Mashabiki kutumia vuvuzela viwanjani kwani inaondoa usikivu kwa wachezaji. Hali hii ilikuja baada ya kuona majukwaa ya Viwanja vya Peter Mokabha,Ellis Park, na vinginevyo kama Royal Bafokeng kule Rosenberg kushambulia sana vuvuzela. 

Kocha wa timu za Vijana nchini, Kim Poulsen


Hoja ya Hispania haikuweza kufanikiwa kwa FIFA na Wasauzi wakaweza kuishuhudia Woza kwa mizuka ileile.Hapo ndipo utakapojua mafanikio yako wako ambao wanaweza kuyatolea macho na kutamani wewe upate matatizo nao wachukue faida ya kufanya ushawishi kwa vyombo husika na kuchukua nafasi.

Watu wasiojulikana Mimi nachukulia kama matatizo yaliyoibuka nchini. Watu hao wamekuwa matatizo kwasababu hadi sasa hawajaweza kufahamika,ni ngumu na kuhatarisha maisha ya watu kwa kuishi na watu wasiojulikana nchi moja. Lolote linaweza kutokea wakati wowote kwasababu vyombo vyetu vya usalama wame tuhakikisha kuwa hawawajui hao manguli wa matukio.

Katika hali hiyohiyo ambayo sisi tulioko ndani tunaweza kuiona kama ni kawaida lakini atatokea mmoja toka kusikojulikana na kuichokonoa CAF juu ya hali ya Usalama wa raia hapa. Inatokea nchi inachukua matatizo yetu ambayo tuashindwa kuyatatua kwa kuyakimbiakimbia na kuona kama hali yeti kiusalama ni ndogo hivi hata Wageni watakao kuja kushiriki AFCON ya U 17 kutilia shaka Usalama wao wawapo nchini.

Yako mataifa ambayo yaweza kuchukua mapungufu yetu na kutaka kujinufaisha.Nani alitegema Leo hii Mashinadano ya Chan yakahamishiwa Morocco badala ya Kenya aliyekuwa mwenyeji wa kuandaa fainali hizo? Umewahi kujiuliza kwanini Caf wamehamisha fainali hizo toka Kenya hadi Morocco? 

Huwezi kutumia akili kubwa kutambua sababu kuu na ya msingi. Tatizo lililojitokeza katika uchaguzi wa Kenya umefanya Chan itoweke Kenya. Hii ndo hoja kuu kwasababu historia ya Kenya katika masuala ya uchaguzi imekuwa imekuwa yenye kurejesha kumbukumbu kubwa kwa wadau wa soka.
Ikiwa uchaguzi wa Kenya ukihairiahwa na kupangwa tena. Caf wanajaribu kufikiria matokeo ya pili yatachukuliwaje kwa wakenya kwa ujumla. Je utulivu wa wakenya utakuwepo kweli ambao unaweza kufanya kusitokee na changamoto yoyote baada ya uchaguzi.

Hili lililomkuta Kenya ndilo lililomkuta Libya aliyetakiwa kuandaa AFCON mwaka 2015 lakini hali ya kiusalama ikafanya kuwe na changamoto na Caf wakaamua kupeleka mashindano Morocco ambako baada ya mlipuko wa maambukizi ya Ebola wakaamua kujiweka pembeni.Ndipo Guinea ya Ikweta ikaamua kuchukua jukumu kuokoa jahazi ikiwa imetoka kuandaa kwa kushirikiana na Gabon miaka mitatu iliyopita yaani 2012.
Tanzania mwaka 2019 itaelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa. Na kwa jinsi hali ya kisiasa ilivyo nchini watu watatumia nafasi hiyo kuelezea hali ya nchi ilivyo wakiwa na mihemko tofauti tofauti. Mara ifikapo tu 2018 tayari kila mwenye matarajio atakuwa anajipanga ili kuweza kulikabili jukwaa la siasa mwaka 2019.
Kama kamata kamata inaendelea kwa haya yanayoendela katika majukwaa ya siasa kinachojengwa katika mioyo ya watu ni chuki na watu watafikia hatua kuwa vibaraka wa Caf na kuharibu Mipango ya sisi kama nchi kuandaa AFCON U17 2019.
Matatizo ambayo yamewapata wakenya imekuwa manufaa kwa Wamorocco. Jambo pekee ambalo linaweza kufanya nchi yetu kwa kutumia watu wenye mamlaka kuweka sawa hali
ya kimifumo ya utawala na kuvutia wengi kuja.

Kama tunategemea kupata wageni watakao leta fursa ya nyongeza ya pato la taifa tunapaswa kujidhatiti na usalama. Hoja ya kutoa majibu ya kusema watu hawajulikani inafanya watu kuweka akiba ya kauli hizi na kuzitumia katika kupora nafasi yetu.
Kama waziri alitolewa bastola na Leo aliyefanya hilo tukio hajulikani inafanya tuonekane tusio makini. Kuondolewa kwa umakini wetu ndiko kutasababisha wengine kuchukua faida na kuhitaji kupora uenyeji wetu.
Tanzania hatujawahi kuandaa mashindano yaliyochini ya CAF badala yke tumefanya hayo kwa ngazi ya Cecafa. Mashindano makubwa kwa umri wa miaka nchini 17 kutahitaji 'support' ya serikali katika kufanikiwa uaandaaji wake.
Usalama wa raia ndio unaotoa ujumbe wa maisha wanayoishi watu katika nchi yao. Sio jambo dogo kuona nchi inafanikisha uaandaji wa mashindano kwani hali ya utulivu na kushiriki kwa serikali ndio mafanikio ya maandalizi hayo.
Tutumie majukwa yetu vyema ili tusitengeneze vinyongo kwa ambavyo vitatufikisha 2018 na kutokuwa na uhakika wakuandaa U17 kwa mwaka 2019. Wasiojulikana inabidi wafuatiliwe na kujulikana ili kuweka mambo sawa.
Matatizo hayakimbiwi bali watu hukaa chini na kufanya uchunguzi hatimaye kubaini Yale yenye kuonyesha uvunjifu wa amani. Kuyafumbia matukio ambayo yanahusu kuondoa usalama wa raia utatoa faida kwa mataifa mengine.Faida ninayoijadili hapa ni uenyeji wa fainali za vijana chini ya miaka 17.
Tuna ya kujifunza kwa kilichotokea Kenya kupokonywa uenyeji wa michuano ya Chan mwaka 2018. Tusijivike gunia na kujifanya hatuoni tunachotakiwa kuwajibika nacho ili kulifanya taifa liwe kama sehemu ambayo wageni hufurahia kuwepo.
Michuano hiyo ni sehemu kutangaza Utalii na vivutio vya vilivyoko katika taifa letu.Utulivu wa miji kama Arusha na ukafanikiwa kuliweka kundi mojawapo la timu kutumia uwanja wa Shikh Amri Abeid unaweza kufanya ongezeko la hamu ya wageni kutamani kuja katika nchi yetu. Lakini ili kufanikiwa hilo tunahitaji utulivu na kukoma kwa matukio yanayoibuka na kukosa ufumbuzi wa vyombo vya usalama.

Www.lundunyasablogspot.Com
0628994409


No comments:

Post a Comment

Maoni yako