October 08, 2008

mwanamke auawa kwa kupigwa shoka

Na HAPPY KULANGA, SONGEA.

Watu wawili wameuawa kikatili katika matukio mawili tofauti yaliyotokea wiki jana.Kamanada wa polisi Falhum Mshana alisema jana kwamba katika tukio la kwanza agnes Kabanda aliuawa kwa kukatwa na shoka kichwani na hawara yake aliyehamika kwa jina la Ally Makinda. Kamanda huyo alisema tkio hilo lilitokea oktoba 3 saa 3:15 usiku katika eneo la Majengo Kisiwani ambako Makinda alimkata mpenzi wake shoka na kukimbia.

Taarifa z akufa zilitolewa na Hassan Salum(28) mkazi wa majengo C ambaye alikuwa akipita nyumbani kwake na kuona mwili wa marehemu ukiwa katika uwanja wa nyumba ya Makinda. Alisema chanzo cha mauaji ni ugomvi uliokuwepo baina ya marehemu na mtuhumiwa, ingawa alisema hadi sasa polisi bado hawajui ugomvi huo ulisababishwa na nini. Lakini uchunguzi unaendelea.

Pili, KILOSA MBAMBA BAY.
MkaZi wa Kilosa katika mji wa Mbamba bay Meshack Ngalima(62) amefariki dunia baada ya kudondokewa na mwembe aliokuwa akiuka. Tukio hilo lilitokea oktoba 3 saa 5 asubuhi mwaka huu. Meshack alifariki muda mfupi baada ya kufikishwa katika kituo kidogo cha afya Mbamba bay alikopelekwa na mdogo wake kwa ajili ya matibabu.

4 comments:

 1. Hapo ipo kazi kweli kweli kwa hiyo hapo kinachobidi kila mtu awe na wake. Sasa naona Songea imeharibika mpaka naogopa.

  Pole wafiwa wote.

  ReplyDelete
 2. unaogopa nini dadangu? mmm mbona ulanzi huogopi? unajua nimeamua kuchukua matukio tu yale ambayo yanayoonyesha akili za binadamu wenzetu zilivyo. nimefanya hivyo ili kujaribu kufanyia utafiti na namshukuru dadangu Happy Kulanga kwa kuniruhusu nitumie habari hizi. ni suala la kujiuliza tu kwanini haya yanatokea?

  ReplyDelete
 3. naona sasa mtakuwa mmenisoma au vipi watu wangu ninavyo wapenda wanyasa miye

  ReplyDelete
 4. usiogope sana kwani naandika haya kwa kutaka kupa tafakari mpya

  ReplyDelete

Maoni yako