January 08, 2009

Maisha! maisha! maisha

Duhh! jamani wakati fulani pale mji wa Mzuzu-Malawi, nilijiuliza mambo kadhaa kuhusu maisha yetu. Samahani usiwaambie uhamiaji kama situmii pasipoti wala mayai visa, maana wale ni ndugu zetu bwana tunalonga kinyanja na kuingia kwa mitumbwi poa. Haya maisha ya Bongo na kule naweza kusema aheri kwetu japo kwa sumuni. Jamani nakumbuka baadhi ya vijiji au mitaani tu wapo wanaoamini Wabongo maisha tunapeta, lakini sote tunajua kinachoendelea. Sasa kwa kawaida huwa najiuliza sana maisha yetu hapa kijijini Lundu na haya ya ndugu zangu wa damu kule Mzuzu na maeneo mengine! Jamani maisha! maisha! maisha! maisha! maisha! maisha!

4 comments:

  1. Maisha Magumu!Pale mikocheni TPDC flats kulikuwa na ma housegirl na ma houseboy kibao wanatokea Malawi. Niliowazoea walikuwa wanakiri kuwa kilichowaleta Tanzania ni tetesi kuwa maisha Tanzania ni rahisi kuliko Malawi. Ila wengi walikujastukia hali halisi. Kuna kipindi kulikuwa mpaka na ugomvi kati ya wafanyakazi wa kimalawi na wakiTZ kutokana na WakiTZ kudai Wamalawi wanashusha mishahara na kufanya kazi sana:-(


    Mzee wa Nyasa nahisi ukigombea urais kuna watakaodai wewe sio MTZ:-)

    ReplyDelete
  2. Duh! kaka Simon kwa kweli maisha ya Malawi baadhi yao wanaamini kuwa TZ poa sana, wengine wamehama kwao na kujichimbia katika hata vijiji vya kando ya ziwa nyasa. wapo wanaoamini kuwa maisha yao Malawi siyo mazuri lakini nashindwa kuelewa walitumia vigezo gani. Enzi zile watu wanatoka Nkata bay, na maeneo fulani ya Mzuzu wanajikita Mbamba bay au Liuli. Rafiki yangu mmoja mtangazaji RADIO TWO FM aliwahi kunieleza hilo, lakini nilikataa nikasema ashuhudie mwenyewe siyo simulizi. Kwakuwa hana shida sana akajaribu kuingia hadi huko DSM, akasema mwanangu sivyo ila tunatakiwa kuhangaikia maisha. Yaani kwa Malawi utaona wakiona mTZ wanajua mambo swadakta kumbe beki hazikabi jamani.

    Kuhusu hili la kudaiwa siyo mTZ, hilo naona watasema lakini sheria zinanilinda, mimi mzaliwa wa TZ nina uraia wa TZ. Ukifanya utafiti wa wapi wanatokea akina MPANGALA jibu lake ni Lilongwe ambako wengi wao wanaitwa MPANGALALA yaani waliopo TZ wameondoa LA moja, ni sawa na akina NGALOMBA. Hizi ni jamii zilizotokea pale, mimi nilipata kwa kutafiti hasa kiini cha ukoo huu. Hapo sijakwambia kuhusu maza, yeye mamake(bibi) katokea Msumbiji kule Beira akaolewa bongo. patamu hapo mkuu

    Mmmmmm mimi MTZ bwana usije ukaniripoti huko TPDC mmm halafu pale jirani na hiyo kuna DR. G. SWAI rafiki yangu sana.

    ReplyDelete
  3. Kumbe kaka Mubelwa alivyomnukuu Lucky Dube katika wimbo wake wa 'the other side' hakukosea. Wao wanadhani kwetu ni afadhali. Nasi tunadhani kwao ni greener zaidi yetu.
    Lakini jina si tatizo kwa leo. Gombea kwanza urais, halafu vurunda, uone. Lakini Ino Galinoma alisema, 'tokea enzi za kale,
    enzi za mababu,
    tuliishi pamoja kama ndugu.'
    wao ndo wametugawa hata leo tumekuwa Tanganyika oh sori, Tanzania au Malawi.

    ReplyDelete
  4. Maisha upande wa TZ ni rahisi sababu kila kitu kinakwenda (biashara). Mie nimeishi MALAWI miaka 17.. napendelea kuishi TZ sababu mambo yanaenda kirahisi na fasta fasta. Kuhusu kabila mbona wengi tu walitoka Malawi na wanajulikana watanzania? Mzee wetu Kawawa wazazi wake ni wamalawi pure. Bado wengine wengi serikali ya Mwalimu kama vile kina mzee Kamaliza aliyekuwa waziri kipindi kile.. wote kina marehemu Shaba aliyewahi kuwa mbunge.. Bado Col. Kayisi ambaye amekuwa mkuu wa mikoa sana miaka ya nyuma....yani nikiorodhesha ni wengi mno. Na hata visiwani Zanzibar kwenyewe wanaojiita waunguja baadhi ya vikongwe wanakwambia wazee wao wanakwambia walitoka Malawi hasa maeneo yenye uislamu kule Likoma na kisiwa cha Salima ziwa Nyasa. Raisi Kaurume aliyeko madarakani sasa asili yake huko.. akiwa mtoto aliwahi someshwa nchini Malawi, na yeye pia alipeleka watoto wake kusoma Malawi. Tanzania ni mchanganyiko wa watu mbalimbali kwani hapo zamani tulikuwa wamoja.

    ReplyDelete

Maoni yako