January 07, 2009

Koero: Maoni yako yananitekenya sana

Rafiki yangu anisomaye sana kaanieleza dada Koero kaweka maoni matamu sana, yanahuzunisha na kufikirisha sana. Nisomapo maoni yako dada Koero yananitekenya sana najiuliza maswali kadhaa ikiwemo Je tutaweza kuibadilisha jamii hii? Je tutaweza kuwafanya watu watamani kusoma vitabu? Nikamkumbuka rafiki yangu Ezdeny Jumanne aliwahi kuweka vijisenti katika kitabu cha How to be Brilliant, akakisahau mahali ambapo alikaa binti fulani lakini wala hakushughulika mpaka tuliporejea na kukitwaa kisha kumweleza mbona anaacha japo hela ya soda? akastaajabu, tukamwonyesha vile visenti akajilaumu sana na kusema kwa utani 'ningejua nakwambia msingekikuta' ..... lakini rafiki yangu Ezdeny Jumanne akasema 'ukitaka kuficha hata hela tu, basi weka kitabuni mbongo hatajua kabisa" Maneno haya yananikumbusha maneno ya kaka Bwaya na wengine LAKINI maoni ya dada Koero yamenitekenya sana na kukumbuka miswada yangu ya 1. LAZIMA UNIOE na 2. TAIFA MOJA, MTAZAMO MMOJA? jamani nimeona niyaweke maoni yake hapa bila kuhariri lolote, nimeyapenda yananigusa kila kona ya mwili DUUH!!!!


Koero Mkundi said...
Kuandika vitabu sawa, lakini wasomaji wapo?
T
atizo ninaloliona ni kwamba watanzania hawapendi kusomavitabu, naomba nikiri hilo, ajitokeze mtu anibishie.
sisi tumekuwa ni jamii ya kupiga majungu, fitna, uwongo, kusengenyana na kuhujumiana.

Tumekuwa ni wavivu wa kufikiri, na hatuko tayari kuongeza maarifa, utakuta mtu kama amesomea mambo ya sheria au udaktari basi yeye na taaluma yake hiyo hiyo hahitaji kuongeza chochote wala kusoma maarifa ya wengine ili kupanua wigo wake wa uelewa, hana muda huo, sana sana labda atazungumzia siasa basi kamaliza.

magazeti yanayopendwa ni ya udaku yale ya hard news hayananafasi na ndio maana yanachechemea, watu hawataki kuyasoma.

Ndio sababu waandishi wengi mahiri hawaandiki tena.
Wako wapi kina Kajubi Mukajanga, Elvis Musiba, Penina Mhando, na wengine nimewasahau.

nashukuru baba yangu alitujengea utamaduni wa kupenda kusoma vitabu mbali mbali bila kuchagua.

06 January, 2009

4 comments:

 1. Maoni ya Dada Koero ni kweli!:-(

  Lakini tusikate tamaa, bado tupo wasomaji na labda swala ni jinsi ya kurudisha usomaji katika fasheni. Kwa maana kuna mambo kibao hata magumu unaweza kumkuta sista du na brazameni wavivu , hawakosi kama tu hicho kitu kikiwa kinatazamwa kama baab kubwa.

  Hata kwenye maswala ya blogu za maandishi, kuna baadhi ya washikaji wajuao huwa sikosi kamera popote nilipo wakawa wananishauri nisiandike badala yake niwe na blogu ya picha kwa sababu ndizo blogu ambazo ndio hutembelewa zaidi na wa TZ!

  Kwa hiyo bado utaona kuwa hili tatizo haliko kwenye vitabu tu , lipo mpaka katika blogu.Uzuri tupo bado tusomao.

  ReplyDelete
 2. Wabongo ni noma hawana nafasi ya kukamua vitabu wala nini mwanangu bali mahaba tu. Blogu za picha sometimes zinaboa mktu wangu utakuta picha maelezo yaani inakuba sana. lakini blogu ya maandishi inachimba inachumbua. washkaji vijiwe vyenu vimetulia ile mabaya yaani mtu akitaka kunitoa mkuku hapa namchoma bisibisi ya kichwa ooohhooo

  ReplyDelete
 3. Kaka Simon kuna wakati naona kabisa blogu za picha zinaboa bwana. Yaani unaangalia picha tu halafu tunadanganywa zina maneno elfu moja. sawa, lakini blogu za maandishi ni muhimu sana tena sana. ndiyo maana nashindwa sana kuweka picha tu bila kuandika maelezo au siku nyingine kuandika tu. Ni muhimu sana blogu za maandishi. ni muhimu sana tena sana.

  ReplyDelete
 4. Nimekusoma kaka Mpangala.

  Huo ulikuwa ni mtazaamo wangu usije ukaacha wadau wakalanijengea chuki.

  ReplyDelete

Maoni yako