August 18, 2017

MFAHAMU MREMA ALIYEUA MAMBA 607 ZIWA NYASA

NILIBAHATIKA kufanya mahojiano miezi sita kabla ya kifo chake Mstaafu wa JWTZ John John Mpembo maarufu kwa jina la MREMA (pichani) ambaye hawezi kusahaulika na wananchi mwambao mwa ziwa Nyasa mkoani Ruvuma baada ya kufanikiwa kukomesha tatizo la mamba kuua watu lililohusishwa na imani za kishirikiana ambalo lilikithiri hasa katika maeneo la Liuli na Mbambabay.
Matukio ya mamba kuua watu yalipungua baada ya kujitosa kwa Mrema kuanzia mwaka 1992 alifanya operesheni kabambe ya kuwaua mamba kwa kutumia ndoana maalum iliyowekwa nyama ya mbwa na aliniambia alifanikiwa kuwaua mamba 607 na kukomesha tatizo hilo.
Mstaafu huyo wa JWTZ aliniambia,Wizara ya malisili na utalii ilikubali kutoa kibali cha kuwaua Mamba katika ziwa Nyasa baada ya vitendo vya mamba hao kukamata na kuua watu kuongezeka na kuleta hofu kwa wananchi ambapo mwaka 1991 mamba hao walidiriki kuwakamata raia wa kigeni ambao walikuwa wanafanya uvuvi wa samaki wa mapambo katika ziwa Nyasa eneo la Liuli.Sasa mambo ni shwari kwa wananchi mwambao mwa ziwa Nyasa imebaki story tu.
Wataalam wanasema kuna aina 15 za mamba,inadaiwa mamba anaweza kuishi kati ya miaka 70, 150 hadi 300,wana urefu unaofikia hadi meta saba, ana uzito wa zaidi ya kilo 1000 na anakula mara moja kwa wiki kati ya kilo 20 hadi 25.

©Albano Midelo, 2017

No comments:

Post a Comment

Maoni yako