December 09, 2008

Najua unanogea+mate yanatoka=urudi nyumbani

najua kabisa unanogea, najua nakupatia HAMU. maana najua bila hamu huwezi kukumbuka kitu. Hawa siyo sawa na dagaa kigoma wanaochacha kama wa enzi zile za KIGONSERA a.k.a CAIGO BOYS, umenisoma kaka Mtanga ha ha ha ha Nina HAMU ndiyo ndiyo maana nakwambia haya. Watazame walivyoanikwa mchangani vizuri halafu unapata NG'ONDA upo hapo. RUDI NYUMBANI ha ha ha ha ha

11 comments:

 1. hata ukijitahidi kunitamanisha kama nini niwuya ngó utajiju. ha ha haaaaa. kazi kweli kweli eti sipa sipi

  ReplyDelete
 2. Kigonsera? Nshasoma na bwana mmoja matata sana. Kichwa cha sumaku. Basi bwana stori za Caigo zilikuwa hazimwishii. Umenikumbusha mbali.

  Halafu kuna mwalimu mmoja wa tuisheni ya Kemia, almaarufu Mkandawile enzi za tuisheni hapo Makongo. Kipindi kikiisha hajawasema madogo wa Caigo tulikuwa tunajua iko problem.

  ReplyDelete
 3. kwali wamwene te tilya sipa mpaka kuhila makunda, yaani "vanibela heee, vanibela heee, vanibela aaaaa wanawake wabaya aaaaaaa. vanibela heeee vanibela heeee vanibela aaaa vambomba vabaya aaaaaa"
  yaani tunaimba na kula, UTAJIJU wewe najua ROHO inauma ha ha ha ha ha ha ha ha huyoooooooooo tumcheke kwanza hooooooooooo

  ReplyDelete
 4. Duuu! CAIGO ni noma unajua pale tumefanya sana kambi za UMISETA mkuu yaani kuna vitu fulani navikumbuka kiasi kwamba ile UMISETA ya mwisho mwaka 2000 ilikuwa inanifanya nicheke sana,kuna vitu fulani vinaitwa VIMBOLO eeeh bwana eeeh yaani vinatengenezwa kama maandazi fulani hivi lakini yakuwa kama fito au unene wa dole gumba halafu virefu. Mkuu nilikuwa nashangaa sana si unajua kwetu nyasa tuliozea dona halafu tunasaka na samaki? basi mambo ya chai viazi MBATATA ile mbaya halafu kwenda kuiba sana mashamba ya wanakijiji pale LUNDO sec. Duu ilikuwa noma, sasa KIGONSERA bwana ina taito kubwa sana lakini mimi nakumbuka mambo ya VIMBOLO au yeyote aliyekuwepo mwaka 2000 UMISETA ile ya mwisho kabla serikali haijafanya ujuha. Duu ilikuwa bomba sana yaani imenikumbusha mbali sana tena ile shule ipo sana katika moyo wangu maana uwezo wangu wa soka ulinifanya niwe pale daima.
  Sasa kaka Fadhy Mtanga akasema kwamba hakuwahi kupenda dagaa lakini najua alichanga mambo maana dagaa wa nyasa ni habari nyingine lakini wale walikuwa akitupikia pale CAIGO ni noma yaani mpishi anakomba jasho anamwagia kwenye pipa la DONA mmmm lakini tulikuwa tunaswinda hivyo huku mazoezi makali sana uwanjani, we fikiria asubuhi unazunguka uwanja raundi 20 halafu mchana saa tisa raundi 15 halafu unashindia DONA na uji fulani. hayo kwa wanasoka unaua kabisa uwezo maana dona siyo mchezo Mkuu
  Ngoja nikomee hapa!
  kaka Fadhy Mtanga upo? usimsikilize dada YASINTA atakoma na mimi safari hii mpaka aondoke huko Uswidi arudi nyumbani DAGAA sana

  ReplyDelete
 5. ha ha ha ha haaaa! nani kakuambia mi nipo uswidi kwali wa mwene nipo nimejaa na nawatwanga tu dagaa tena ligánda, halafu magege ya kuchoma ambayo yamepakwa chumvi na piliåili na gwali gwa mayahu. Kunyumba nga kunyumba haha hhaaaaaaaaaaa

  ReplyDelete
 6. haya utaishia kunawa tu kula hili!!!! ha ha ha ha mpaka urudi kwenye mstari wa nyasa. huyoooooo ha ha ha ha ha ha ha

  ReplyDelete
 7. kama huamini basi shauri yako wewe uliye huko darislam mi nipo hapa kwetu rihiwiko jana tu nimerudi kutoka kunyanja. utajiju

  ReplyDelete
 8. Wannala veve udeseogo! kwe kuruhuwiko kuna nini? KANYANJA utarudi tu ha ha ha ha ha ha muone tabasamu lake meno meupeeeeee lakini dagaa hakuna utajiju leo ha ha ha ha ha

  ReplyDelete
 9. Nipo nipo kama kawa, vimbolo vilikuwa vitafunio babkubwa.
  Sikuwapenda wale dagaa sababu ya maandalizi yake.
  Sasa hivi ni mboga niipendayo kuliko. Kwa taarifa yako hapa ndo nimemaliza kula ugali na dagaa, ila hawa ni wa Kigoma. Nimebakiza kimtindo, ntawapikia ubeche jioni.
  Shauri lako da Yasinta unaetokwa na mate mdomoni.
  Kigonsera. Shule ile kaka iache tu kama ilivyo.

  ReplyDelete
 10. Hey whats up man? hallow Guard Runner u are WELCOME karibu nyasa mkuu maana ung'eng'e umenishinda bwana

  ReplyDelete

Maoni yako